ABUJA : Wanigeria waonywa dhidi ya ghasia | Habari za Ulimwengu | DW | 13.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ABUJA : Wanigeria waonywa dhidi ya ghasia

Rais Olesegun Obasanjo wa Nigeria amewaambia Wanigeria hapo jana kupunguza safari zao wakati wa siku za uchaguzi zinazokuja na kubakiwa nyumbani wakati wa usiku ili kuzuwiya ghasia na hujuma.

Obasanjo amewashutumu watu walioko kwenye nafasi za juu kwa kuchochea vurugu kabla ya uchaguzi wa tarehe 14 hadi 21 mwezi wa April na chama kikuu cha upinzani kimesema wagombea wake kadhaa na maelfu ya wafuasi wao wametiwa mbaroni.

Obasanjo amesema katika radio na televisheni ya taifa kwamba wakati wa siku ya uchaguzi nyendo ziwe kwa lisilokuwa na budi tu.

Zaidi ya watu 100 wamekufa katika vurugu zinazohusiana na uchaguzi nchini kote Nigeria tokea mwezi wa Novemba mwaka 2006.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com