ABUJA: Mfanyakazi wa Kifilipino atekwanyara Nigeria | Habari za Ulimwengu | DW | 06.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ABUJA: Mfanyakazi wa Kifilipino atekwanyara Nigeria

Nchini Nigeria watu wenye silaha wamemteka nyara Mfilipino alieajiriwa na kampuni ya mafuta-Shell na wamemuuwa askaripolisi aliekuwa akimsindikiza mfanyakazi huyo wa kigeni katika eneo la Niger Delta.Mtaalamu wa usalama katika kampuni moja kuu ya mafuta amesema,shambulio hilo lilitokea kwenye barabara inayoelekea Port Harcourt katika eneo lenye utajiri wa mafuta.Mwezi uliopita,serikali ya Ufilipino ilitoa amri kwa wizara yake ya ajira kutowaruhusu wafanyakazi kwenda Nigeria,baada ya mabaharia 24 wa Kifilipino kutekwa nyara katika Niger Delta.Watu hao wapo kizuizini hadi hii leo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com