1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ABUJA: Mfanyakazi mfilipino aachiliwa huru

Polisi nchini Nigeria wamesema mfanyakazi wa kampuni ya mafuta raia wa Ufilipino aliyetekwa nyara mnamo tarehe 6 mwezi uliopita katika eneo la Niger Delta kusini mwa Nigeria, ameachiliwa huru na kukabidhiwa kwa waajiri wake.

Watu waliokuwa na bunduki walimtekanyara mwanamume huyo katika barabara inayoelekea mji wa bandari wa Port Harcourt na kumuua afisa mmoja wa polisi aliyekuwa miongoni mwa maafisa wengine waliokuwa wakimsindikiza mfilipino huyo.

Kamishna wa polisi wa jimbo la Rivers amesema mfilipino huyo aliachiliwa huru jana lakini hakutoa maelezo zaidi juu ya masharti ya kuachiliwa kwake.

Mpaka sasa wafanyakazi saba raia wa kigeni bado hawajulikani waliko tangu walipotekwa nyara katika eneo la Niger Delta.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com