1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABIDJAN: Serikali ya mpito yatangazwa Ivory Coast

8 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBa

Ivory Coast imetangaza serikali mpya ya mpito,kwa azma ya kuitayarisha nchi hiyo kwa chaguzi huru na za haki.Katika juhudi ya kutaka kuiunganisha nchi,serikali mpya inawaleta pamoja waasi wa zamani na washirika wa Rais Laurent Gbagbo. Serikali hiyo imeundwa kufuatia makubaliano ya amani ya tarehe 4 mwezi Machi,kati ya Rais Gbagbo na kiongozi wa waasi Guillaume Soro.Tangu mwaka 2002,Ivory Coast imegawika sehemu mbili,baada ya jeribio la Soro la kutaka kuipindua serikali kushindwa kufanikiwa.Tangu wakati huo,vikosi vya Soro vimedhibiti eneo la kaskazini huku majeshi ya Gbagbo yakidhibiti sehemu ya kusini.Soro,sasa amefanywa waziri mkuu katika serikali mpya ya mpito.Kwa mujibu wa serikali hiyo,vikosi vya kigeni vinavyolinda eneo lililo kati ya kaskazini na kusini vitaanza kuondoka ifikapo katikati ya mwezi huu.