ABECHE:Waandishi wa habari na wahudumu wa ndege huenda wakaachiwa | Habari za Ulimwengu | DW | 02.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ABECHE:Waandishi wa habari na wahudumu wa ndege huenda wakaachiwa

Rais wa Chad Idriss Deby anataraji kuwa waandishi wa habari wa Kifaransa na wahudumu wa ndege ya Uhispania wanaozuiliwa huenda wakaachiliwa ila sheria sharti zidumishwe. Wafanyikazi hao wa shirika la msaada pamoja na waandishi wa habari huenda wakatumikia kifungo kinachoandamana na kazi ngumu kwa kupatikana na hatia ya kuwateka watoto hao huku wahudumu wa ndege wakishatkiwa kwa kuhusika na njama hiyo. Kiongozi huyo wa Chad anathibitisha kuwa amewasiliana na rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na kuongeza kuwa sharti kazi ya waandishi wanaozuiliwa itengwe na shughuli za shirika la kutoa misaada kwa watoto Zoe’s ARK.

Kulingana na Shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na watoto UNICEF watoto hao walikuwa si yatima kamam ilivyodaiwa na Shirika la Zoes Ark.Leila Blacking ni afisa katika shirika la msaada la msalaba mwekundu Redcross

''Imeshathibitishwa kuwa watoto 91 kati ya wote 103 wana jamaa au mtu wanaomtambua kama mzazi.Imebainika kuwa huenda wana jamaa zao. ''

Waendesha mashtaka nchini Chad wamewashtaki watu 17 wa Ulaya na wawili wa Chad kwa madai ya kuwateka au kuhusika na mpango mzima wa kujaribu kuwasafirisha watoto 103 wa Kiafrika kutoka Abeche hadi Ufaransa.Shughuli hiyo ilifanyika tarehe 25 mwezi Oktoba huku shirika hilo la Zoe’s Ark likidai kuwa linawaondoa watoto hao kuepuka ghasia katika eneo la Darfur nchini Sudan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com