1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

96 WAFARIKI MSUMBIJI

24 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFw

MAPUTO:

Idadi ya waliofariki kutokana na miripuko kadhaa katika ghala la siasa nje ya mji mkuu wa Msumbiji (Maputo) imefikia 96.Kuna hofu za kuzuka miripuko mingine kutokana na joto kali.

Waziri wa afya wa Msumbiji, Ivo Paulo Garrido ametangaza siku 3 za maomblezi.Watu wengine 400 wamejeruhiwa.Nyumba kadhaa zimeteketezwa na makombora yalioruka na kufikia hadi km 10 kutoka ghala ilipo.Mamia ya watu bado hawajulikani walipo baada ya kuikimbia miripuko hiyo pamoja nao watoto wadogo.Polisi wakiwaarifu wakaazi wa maeneo yaliohamishwa wakaazi wasirejee makwao kwa siku kadhaa ikihofiwa hali ya joto kali yaweza ikasababisha miripuko mipya.