George Weah ameshinda kwa wingi mkubwa uchaguzi wa rais nchini Liberia// Uganda imewafungulia mashitaka ya ugaidi raia 45 wa Rwanda baada ya kukamatwa katika mpaka wa Uganda na Tanzania mapema mwezi huu// Mahakama ya juu ya Afrika Kusini leo imetoa hukumu kwamba bunge la nchi hiyo limeshindwa kumuwajibisha ipasavyo Rais Jacob Zuma juu ya kashfa ya kutumia fedha za umma.