20 WAUWAWA IRAK
24 Machi 2007Matangazo
BAGHDAD:
Lori la mtu aliejiripua lilihujumu leo kituo cha polisi mjini Baghdad na kuua watu 20 huku magari 3 ya waliojitolea mhanga wakati mmoja yalihujumu kituo cha njiani ya ukaguzi magharibi mwa Iraq.
Miongoni mwa watu 20 waliouwawa katika hujuma ya kituo cha polisi huko Dora wanajumuisha polisi 14 na wafungwa 3 waliokua wakifanya kazi katika jengo hilo.Watu wengined 26 wsamejeruhiwa wengi wao ni polisi.