1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

14 wauwawa Irak

9 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRE

BAGHDAD:

Si chini ya wairaki 14 wameuwawa katika hujuma 2 mbali mbali asubuhi ya leo katika miji ya kaskazini ya Kirkuk na Tikrit-polisi imearifu.

Na katioka kijiji kiliopo kusini-magharibi mwa Kirkuk, na km 250 kaskazini mwa mji mkuu baghdad, vikosi vya Irak vilivurumisha makombora katika kundi la waasi na kuwaua 7 kati yao.Vikosi hivyo vilisaidiwa na vile vya Marekani.

Katika tokeo jengine, Irak na majirani zake Iran na Syria walkikuwa n a mkutano mapema leo asubuhi wa nc hi hizo jirani kuzungumzia hasa matatizo ya mkoa huo pamoja na yale ya nishati,usalama na ya wakimbizi wa Irak.