Karibu kwa Jarida la habari la DW.COM Tafadhali jisajili hapa.
Yaliyomo katika matangazo ya Jioni: Migogoro ya Gaza na Ukraine kujadiliwa katika mkutano wa jukwaa la kiuchumi mjini Riyadh Saudi Arabia++++Mafuriko yasababisha adha kubwa nchini Kenya watu 76 mpaka sasa wamepoteza maisha++++Sheria mpya ya Iraq inayowalenga watu wenye mahusiano ya jinsia moja yakosolewa na mashirika ya haki za binadamu duniani.
Saudi Arabia inakhofia vita kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas vilivyoongeza mivutano katika kanda ya Mashariki ya kati vinaweza kuvuruga hali ya kiuchumi duniani kote
Muhtasari wa matangazo ya mchana: Saudia Arabia yaonya juu ya vita vya Gaza kudumaza uchumi wakati mkutano wa kilele wa jukwaa la uchumi duniani ukifunguliwa mjini Riyadh. +++Kundi la wanamgambo la Hamas limetoa mkanda wa vidio unaoonyesha mateka wanaoshikiliwa. ++++Watu 76 wapoteza maisha katika mafuriko nchini Kenya.