Zverev apeta Madrid Open | Media Center | DW | 14.05.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Media Center

Zverev apeta Madrid Open

Mchezaji Tennis wa Ujerumani Alexander Zverev amelishinda taji la Madrid Open baada ya kumshinda Dominic Thiem kwenye fainali kwa seti mbili za 6-4 6-4.

Zverev mwenye umri wa miaka 21 aliishinda mechi hiyo baada ya saa moja na dakika kumi na nane na anasema kwamba anatumai kwamba ushindi huo utakuwa ni motisha kwake wa kuendelea kucheza vyema zaidi.

Licha ya kuebuka bingwa Mjerumani huyo amekiri kwamba Rafael Nadal na Roger Federer bado ndio wachezaji bora zaidi katika Tennis.

Mwandishi: Jacob Safari/AFPE/DPAE/APE

Mhariri: Iddi Ssessanga