1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zuma achaguliwa rais wa chama.

19 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cdmq

Polokwane.

Waungaji mkono wa Jacob Zuma wanaendelea kusherehekea nchini Afrika kusini siku moja baada ya kuwa kiongozi mpya wa chama cha ANC. Zuma amemwangusha mpinzani wake na rais wa sasa wa Afrika kusini Thabo Mbeki na sasa anaonekana kuwa huenda akachukua nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka 2009.

Huu ulikuwa mpambano wa kwanza viongozi kwa chama cha ANC katika karibu miaka 60 na ushindani baina ya viongozi hao wawili umesababisha mpasuko mkubwa ndani ya chama pamoja na mzozo wa kisiasa nchini humo. Zuma bado anakabiliwa na tuhuma za rushwa zinazohusiana na kashfa ya ununuzi wa silaha.