Zorniger apewa majukumu ya kuiongoza Stuttgart | Michezo | DW | 25.05.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Zorniger apewa majukumu ya kuiongoza Stuttgart

Miamba wa zamani wa Bundesliga VfB Stuttgart ambao wamefanikiwa kusalia katika ligi kuu msimu huu, wamepata huduma za kocha mpya atakayewaongoza msimu ujao

Alexander Zorniger anatachukua usukani kama kocha wa Stuttgart kuanzia msimu ujao, katika jitihada za kuyaweka mambo sawa. Zorniger amechukua nafasi ya Huub Stevens ambaye aliliokoa jahazi la klabu hiyo katika hatua za mwisho mwisho za msimu wa Bundesliga.

Zorniger mwenye umri wa miaka 47 amewahi kufanya kazi na Stuttgart mwaka wa 2009 kama kocha msaidizi, lakini amekuwa akiifunza timu ya ligi ya daraja la pili ya RB Leipzig kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Amepewa mkataba wa miaka mitatu hadi Juni 2018. Andre Trulsen atakuwa msaidizi wake.

Mwandishi: Bruce Amani/RTRE
Mhariri: Yusuf Saumu