1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zoezi la Sudan ya Kusini lasifiwa

18 Januari 2011

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na wasimamizi wa kimataifa, kuhusu kura ya maoni iliyopigwa kuamua hatima ya Sudan ya Kusini, zoezi hilo limeridhisha kwa sehemu kubwa.

https://p.dw.com/p/QtCW
epa02521167 Southern Sudanese men wait in line to vote for the referendum on the independence of South Sudan at a polling station in Juba, Southern Sudan, 09 January 2011. (...) An emotional Salva Kiir, president of Southern Sudan, choked back tears as he cast his ballot and dedicated the vote to independence leader John Garang - who died in a 2005 helicopter crash - and all those who perished in the war. Just under 4 million Southern Sudanese are registered to put a thumbprint on the ballot - either under a picture of two hands clasping for unity, or one held up as if waving goodbye for secession. Few doubt that jubilant and expectant Southern Sudanese will vote for independence, but at least 60 per cent of registered voters must turn out for the referendum to be valid. The vote, which many had doubted would take place on time, has raised fears of a return to conflict between north and south. EPA/MOHAMED MESSARA +++(c) dpa - Bildfunk+++
Wasudan wa Kusini wakingojea kupiga kura.Picha: picture alliance/dpa

Wiki iliyopita, kiasi ya watu milioni nne katika Sudan ya Kusini walipiga kura kuamua iwapo eneo hilo lenye utajiri wa mafuta, lijitenge na Kaskazini. Licha ya kuwepo vitisho vya mashambulio na harakati za kutayarisha kura hiyo ya maoni kuendelea hadi dakika ya mwisho, zoezi hilo lilifanyika kwa amani kinyume na vile ilivyotazamiwa na baadhi ya wachambuzi. Kwa mujibu wa wasimamizi wa kimataifa, kura hiyo ya maoni, kwa sehemu kubwa, ilikwenda kwa usalama. Takriban vituo vyote vya kupigia kura vilikuwa na orodha ya wapiga kura na karatasi za kupigia kura. Maafisa wa uchaguzi pia wamesifiwa kwa kazi nzuri iliyofanywa, lakini kulishuhudiwa pia vitendo vya kuwatisha wapiga kura.

Southern Sudan President and elections candidate Salva Kiir waits to casts one of his ballots at a poling station set in a restaurant in Juba, southern Sudan, Sunday April 11, 2010. The people of Southern Sudan will cast ballots in a national election for the first time in more than two decades as a three-day election begins Sunday. Despite the first-in-a-generation vote, most people are already looking past the elections to a vote next January considered far more significant: a referendum on independence that could signal the birth of a new African nation, if final negotiations with Khartoum over oil rights and the location of the border are worked out peacefully. (AP Photo/Jerome Delay)
Rais wa Sudan ya Kusini, Salva KiirPicha: AP

Idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura katika baadhi ya maeneo ya Sudan ya Kusini ilipindukia asilimia 90. Hiyo ni zaidi ya kiwango cha asilimia 60 kinachohitajiwa ili matokeo ya kura ya maoni yaweze kutambuliwa. Lakini katika kaskazini mwa nchi, ambako wananchi wenye asili ya Sudan ya Kusini walikuwa pia na haki ya kupiga kura, ni wachache walioitumia fursa hiyo. Josef Sayer, mkurugenzi mkuu mtendaji wa shirika la misaada la Kijerumani Misereor alikuwa msimamizi mmojawapo. Anasema, watu walihofia kwamba walikuwa wakitazamwa na vikosi vya usalama. Vile vile hawakuwa na hakika iwapo kura zao zitahesabiwa.

Kwa upande mwingine, Abyei ni eneo linaloendelea kuwatia wasiwasi wasismamizi hao wa kimataifa. Wakaazi wa wilaya hiyo iliyopo kati ya mpaka wa Sudan ya Kaskazini na Sudan ya Kusini, walikuwa wapige kura ya maoni katika zoezi maalum kuamua iwapo wabakie na kaskazini au wajiunge na kusini. Lakini kura hiyo imeahirishwa kwa muda usiojulikana kwa sababu ya mzozo wa kisiasa. Eneo hilo linagombewa na kila upande kwa sababu ya utajiri wake mkubwa wa mafuta. Kwa maoni ya wasimamizi Sudan ya Kusini haitoweza kuunda taifa huru kwa usalama ikiwa hatima ya Abyei haitoamuliwa. Mjumbe wa Umoja wa Ulaya, Veronique de Kayser, amesema:

"Kwa hakika suala la Abyei ndio ufunguo unaowaeza kufungua mlango kwa matatizo mengine. Kwa hivyo, ni lazima litatuliwe katika kiwango cha kisiasa, tena kwa kipaumbele cha juu kabisa. kwani linaweza kusambaratisha eneo zima, ikiwa suluhisho la kisiasa halitopatikana haraka."

Majadiliano kuhusu eneo hilo tajiri la Abyei bado hayakuanza, lakini kura zilizopigwa Sudan ya Kusini zimeshaanza kuhesabiwa. Matokeo ya mwanzo kutoka Juba, mji mkuu wa kusini, yanaonyesha kuwa idadi kubwa ya wakaazi wa eneo hilo wanataka uhuru. Matokeo ya mwisho yanatazamiwa mwezi wa February.

Mwandishi: Pelz, Daniel/ZPR

Mpitiaji:Miraji Othman