ZIMBABWE | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 30.04.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

ZIMBABWE

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kuafikiana juu ya mgogoro wa Zimbabwe.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moonBaraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kuafikiana juu ya azimio kuhusu mgogoro wa Zimbabwe kutokana na upinzani wa Afrika Kusini iliyohoji kuwa mgogoro huo ni suala la ndani ya nchi hiyo

Baraza lilishindwa kufikia tamko la pamoja juunya mgogoro wa Zimbabwe baada ya Afrika Kusini kupinga na kuhoji kwamba mgogoro huo ni wa watu wa Zimbabwe .

Wajumbe wa nchi za Ulaya,Marekani na Latin Amerika walitaka kupelekwa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa.

Mjumbe wa Uingereza aliliambia Baraza hilo kuwa Zimbabwe inakabiliwa na mgogoro mkubwa usiokuwa na mithili tokea nchi hiyo ijikomboe. Mjumbe huyo amesema watu milioni moja na laki tano sasa wanategemea msaada wa chakula.

Hapo awali naibu kiongozi wa chama cha upinzani nchini Zimbabwe alilitata Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lipeleke mjumbe maalumu nchini Zimbabwe kuonesha kuwa jumuiya ya kimataifa ina dhamira ya kuwasaidia watu wa Zimbabwe kutatua masuala ya haki za binadamu,mgogoro wa kisiasa na hali mbaya ya maisha inayowakabili watu.

Lakini baraza la Usalama limeshindwa kuafikiana juu ya hatua ya kuchukua.

Rais wa Baraza hilo amesema sasa ni juu ya katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kuamua juu ya kupeleka mjumbe maalumu au kupeleka ujumbe utakaochunguza hali ya nchi hiyo.

Wakati Marekani,Uingereza na Ufaransa zinataka Umoja wa Mataifa upeleke mjumbe nchini Zimbabwe,Afrika kusini,Urusi ,China na nchi zingine zinapinga wazo la kuchukua hatua yoyote kwa sasa.

Wakati huo huo viongozi wa vyama vya upinzani wanataka matokeo ya uchaguzi wa rais yatolewe nchini Zimbabwe.

 • Tarehe 30.04.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DrA0
 • Tarehe 30.04.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DrA0
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com