Zimbabwe yakabiliwa na njaa | Matukio ya Kisiasa | DW | 10.03.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Zimbabwe yakabiliwa na njaa

Kwa mara ya kwanza Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amekiri kwamba nchi yake inakabiliwa na njaa.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe,alipowasili mjini Lisbon kwa ajili ya Mkutano wa nchi za Ulaya na Afrika Dec. 9, 2007.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe,alipowasili mjini Lisbon kwa ajili ya Mkutano wa nchi za Ulaya na Afrika Dec. 9, 2007.

Mugabe ametoa hiyo kauli wakati ambao Zimbabwe inajiaandaa kwa uchaguzi mkuu wa urais unaotarajiwa kufanyika tarehe ishirini na tisa mwezi huu na yeye akiwwa mgombea wa chama tawala cha ZANU-PF.

Rais Mugabe amekaririwa na gazeti la kila Jumapili linalomilikiwa na Serikali ya nchi hiyo akisema kwamba ni kweli kuna njaa, Zimbabwe inakabiliwa na uhaba wa chakula.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, Rais Mugabe alikuwa akizungumza katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Magharibi mwa Zimbabwe mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mugabe alikuwa akiitikia mwito uliotolewa na Gavana wa Mkoa mmoja wa Maagharibi wa Angeline Masuku na Viongozi wa chama Tawala katika eneo hilo waliomtaka kuhakikisha anaongeza juhudi za kusambaza chakula katika majimbo ambayo wananchi wake hawana chakula.

Wachunguzi wa mambo wamesema kwamba kitendo cha Mugabe kukiri kuwepo kwa njaa nchini humo ni kitenddo ambacho hakijawahi kutokea.

Rais Mugabe amekuwa mara nyingi akipinga taarifa za kuwepo kwa njaa nchini humo na kuziona kama propaganda za Kimagharibi.

Mnamo mwaka 2006, alipoulizwa katika mahojiano juu ya tatizo sugu la upungufu wa mahindi ambalo ni zao kuu nchini humo, Rais Mugabe alisema kwamba wanaviazi vingi sana kuweza kukabiliana na hali hiyo.

Hata hivyo ni mwaka mmoja tu umepita baada ya kauli hiyo, jana amekiri kuwepo kwa upungufu wa chaakula na wala siyo tu katika majimbo makavu yaliyoko Magharibi lakini pia katika maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa Zimbabwe.

Mashirika mbalimbali ya Kimataifa tayari yameshatoa msaada wa chakula kwa watu milioni nne.

Katika kipindi cha joto kilichoweka historia ya mvua kubwa iliyoharibu mazao ya chakula, kilifuatiwa na kipindi kikavu kwa muda wa mwezi mzima katika maeneo ambayo yamekuwa yakizalisha mahindi kwa wingi kitendo ambacho wataalamu wanahofia kwamba huenda uhaba huo wa chakula ukawa ni mkubwa zaidi ambao haujawahi kutokea.

Zimbabwe ilikuwa na sifa ya kuwa na uwezo wa kulilisha bara zima la Afrika kutokana na mavuno mengi ya ziada ya nafaka wakati mashirika ya misaada yalikuwa yakitumia mavuno hayo ya ziada kulisha uma uliokuwa ukikabiliwa na njaa kati nchi za Afrika.

Hata hivyo Sekta ya kilimo ya nchi hiyo ilianza kuyumba katika miaka ya 2000 baada ya Rais Mugabe kuanzisha kampeni isiyokuwa ya kisheria ya kuwafukuza wakulima wa kizungu wapatao elfu nne na mia tano na badala yake mashamba hayo wakapewa wanachama wa chama Tawala.

Jana Rais Mugabe alisema kwamba kiasi cha tani laki tano na thelathini za mahindi zimeagizwa kutoka nchi jirani lakini kutokana na tatizo la usafirishaji mpaka sasa ni tani thelathini elfu tu ndizo zimeshawasili.

Ameahidi pia kwamba kuna traine ambayo itapeka mahindi nchini humo ikitokea Zambia ikiwa ni sehemu ya njia ya kuongeza misaada ya dharura ya chakula kwa wananchi wa kawaida wa nchi hiyo.

Wakati huohuo, Rais Robert Mugabe amekuwa akiendelea na Kampeni yake ya kuwania urais katika uchaguzi ujao, na tayari ameshatia saini sheria mpya ya kuwataka wageni na wafanyabiashara wa kizungu kutoa asilimia hamsini na moja ya shughuli za uendeshaji biashara hizo kwa watu weusi.

Tayari Serikali imetwaa mashamba kadhaa ya wazungu tangu mwaka 2000, lakini wakosoaji wanasema mashamba hayo yamegawanywa kwa wakubwa Serikalinina katika chama Tawala cha ZANU-PF:

 • Tarehe 10.03.2008
 • Mwandishi Scholastica Mazula
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DLvv
 • Tarehe 10.03.2008
 • Mwandishi Scholastica Mazula
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DLvv
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com