Zimbabwe yajiondoa CECAFA Senior Challenge | Michezo | DW | 30.11.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

CECAFA Senior Challenge

Zimbabwe yajiondoa CECAFA Senior Challenge

Zimbabwe imejiondoa katika dimba la Kombe la CECAFA Senior Challenge litakaloanza wiki hii nchini Kenya, wakitaja sababu za kiusalama.

Zimbabwe ilialikwa kushiriki katika kinyang'anyiro hicho kitakachong'oa nanga Desemba 3 hadi 17 kama moja ya timu mbili zilizoalikwa kama wageni pamoja na Libya.

Shirikisho la kandanda la Zimbabwe limesema katika taarifa kuwa hatua ya kukataa mwaliko huo imechukuliwa baada ya mazungumzo mapana kuhusiana na hali ya kisiasa nchini Kenya.

Waandalizi wa dimba hilo wamesema wamehuzunishwa na uamuzi wa Zimbabwe, lakini wakaahidi kuwa mashindano hayo yataendelea kama yalivyopangwa, huku timu tisa zikijipanga kupambana.

Zimbabwe ilitarajiwa kuanzisha kampeni yake ya Kundi B dhidi ya mabingwa watetezi Uganda mnamo Desemba 4 katika mji wa magharibi ya Kenya, Kakamega.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com