1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zimbabwe kupitisha sheria mpya ya ujenzi

11 Mei 2022

Sheria hiyo mpya ni kuhusu ujenzi wa nyumba, ili kusaidia jamii za vijijini ziweze kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

https://p.dw.com/p/4B7Qi
USA Robie House von Architekt  Frank Lloyd Wright
Picha: imago/D. Delimont

Zimbabwe inapanga kupitisha sheria mpya kuhusu ujenzi wa nyumba. Sheria hizo zinalenga kusaidia jamii za vijijini ziweze kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa yakiwemo upepo mkali na mvua kubwa zinazo sababisha mafuriko.

Kulingana na takwimu za serikali nchini Zimbabwe  kuanzia  2017, zimeonyesha  kuwa asilimia 80  ya nyumba katika maeneo ya vijijini zimejengwa  kwa matofali ya udongo ambayo ni mbinu ya jadi , na asilimia 98  ya nyumba katika maeneo ya mijini zimejengwa kwa matofali ya saruji  ambayo ni mbinu ya kisasa.

Florence Panda,  ni raia nchini Zimbabwe anayeishi kwenye nyumba mpya iliyojengwa muundo wa kisasa , baada ya kupoteza nyumba yake ya awali katika  kijiji cha Ndiadzo, huko Jimbo la Manicaland mashariki mwa nchi hiyo, kutokana na upepo mkali na mvua za mafuriko zilizonyesha   Zimbabwe  mwaka 2019, na kuharibu takriban nyumba 50,000.

''Tuliishi kwenye mahema''

Mvua kubwa iliyonyesha ilisomba nyumba ya panda aliyoijenga kwa  matofali ya udongo wa kichuguu  na kusababisha familia ya Panda kukosa makazi.

"Ilikuwa huzuni kupoteza makazi  yetu na kila kitu  kwa usiku mmoja tu,” Panda aliliambia Shirika la habari la Reuters kwa njia ya simu.

"Kwa zaidi ya mwaka mmoja, tuliishi kwenye mahema, tulifurahi kupata makazi mapya kwani ilikuwa ahueni ."

Mwaka mmoja baadaye, Panda na familia yake walihamia kwenye nyumba za kisasa zilizojengwa vijijini  na serikali, zenye viwango vya kuhimili mvua kubwa na  upepo mkali.

Miradi ya serikali kwa wathiiriwa wa majanga

Moderne Sklaverei
Picha: Pete Pattisson

Percy Toriro, mtaalamu wa mipango miji aliyepo  mjini Harare, alisema hii ni awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba za kisasa maeneo ya  vijijini na zitakuwa na ubora kama nyumba za mijini." makazi ya mijini yamekuwa salama zaidi kutokana na udhibiti wa viwango na  ubora nyumba  ambapo, makazi ya vijijini hayakuwahi kudhibitiwa viwango au ubora wowote," alisema.

Mnamo mwaka 2020, serikali ya Zimbabwe ilipitisha sera na sheria mpya ya ujenzi wa nyumba na kujenga nyumba za kisasa 700, kwa watu walioathiriwa na majanga ya asili., alisema Nathan Nkomo, mkurugenzi wa Idara ya  Ulinzi wa Raia, kwenye shirika la  Serikali la kukabiliana na maafa, ambalo lilisaidia kuunda viwango vipya vya ujenzi.

Sera mpya ya makazi, inaitaka mabaraza  ya vijijini kuhakikisha majengo yote mapya ya vijijini yanajengwa kisasa, kwa kuzingatia ubora na viwango vya  kitaifa na kimataifa, alisema David Mutasa,mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makoni Vijijini.

Hifadhi ya mazingira 

Ili kuzuia uharibifu wa  mazingira, sera inapiga marufuku ujenzi wa  vibanda  vya mbao kwenye maeneo ya vijijini  na  ujenzi kwenye maeneo ya bondeni ili kujikinga na majanga ya asili.Nchini Zimbabwe, adhabu ya ukataji miti bila kibali ni kati ya dola 5,000 na 50,000 za Zimbabwe ($13-$133).

Sio kila mtu amefurahia  sera mpya ya makazi, na baadhi ya viongozi wa eneo hilo wamesema wamekabiliwa na shinikizo.Nyumba za jadi, unaweza kujenga kutumia udongo na mbao bila gharama yoyote,alisema Toriro, mtaalam wa mipango.

"Baadhi ya watu hawana fedha za kujenga nyumba za kisasa kutokana na viwango vinavyohitajika,” alisema. Florence Panda ambaye  alitumia $500 kuongeza vyumba vitatu zaidi kwenye nyumba yake mpya iliyojengwa na  katika kijiji cha Ndiadzo.