1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zilzala yatikisa Uchaguzi wa Bunge la Ulaya

26 Mei 2014

Ushindi wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia nchini Ufaransa FN umegubika matokeo ya uchaguzi wa bunge la ulaya huku sauti za wenye kulalamika na wale wenye kuupinga umoja wa ulaya zikipata nguvu pia

https://p.dw.com/p/1C6vB
Makadiroo ya matokeo ya uchaguzi wa bunge la Ulaya kama yalivyotangazwa jana asaa nne na dakika 51 za usiku nchini Ujerumani

Nchini Uingereza chama cha UKIP kinachopigania nchi hiyo ijitoe haraka katika Umoja wa ulaya,nacho pia kimeupindua wizani wa kisiasa na kujipatia ushindi wake wa kwanza katika daraja ya taifa.

Bila ya kusubiri matokeo ya mwisho kutangazwa waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls amesema ushindi wa FN,wanaosemekana kujikingia asili mia 26 ya kura,wakiwapita wahafidhina wa UMP kwa pointi zaidi ya tano na zaidi ya 12 mbele ya chama cha Soshialisti,"ni kishindo,na zilzala kwa Ufaransa na Ulaya kwa jumla."

Idadi ndogo ya wapiga kura,asili mia 43 imevisaidia vyama vyingi vya siasa kali ya mrengo wa kulia na mrengo wa kushoto katika nchi kadhaa ,hata kama nchini Ujerumani ,Italia na Hispania vyama tawala ndivyo viliovyoshinda.

Ingawa wenye kuuangalia kwa jicho la wasi wasi Umoja wa ulaya wanaonyesha kuzidisha maradufu matokeo yao ikilinganishwa na miaka mitano iliyopita,hata hivyo hawatawazuwia wahafidhina na wasosial Democrate kudhibiti bunge la ulaya.

Jean-Claude Juncker asema ana haki ya kuwa mwenyekiti wa Halmashauri kuu

Kwa mujibu wa matokeo ya hadi hivi punde chama cha kihafidhina barani Ulaya ,kinachojumuisha pia chama cha Christian Democratic cha kansela Angela Merkel,na UMP cha Ufaransa kimejikusanyia viti 212 kati ya 751 vya bunge jipya la ulaya.Chama cha kisoshialishi barani Ulaya kimejikingia viti 186.

EU Parlamentswahl 25.05.2014 Juncker
Waziri mkuu wa Zamani wa Luxemburg Jean-Claude JunckerPicha: John Thys/AFP/Getty Images

Mgombea wa chama hicho cha kihadhifa kwa wadhifa wa mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa ulaya,waziri mkuu wa zamani wa Luxembourg Jean-Claude Juncker anasema"Kwakua wao ndio walioshinda,anahisi ni haki yake kuwa mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa ulaya."

Hata hivyo mgombea wa chama cha Social Democrat barani Ulaya,spika wa sasa wa bunge la ulaya Martin Schulz wa chama cha Social Democratic cha Ujerumani anasema hajakata tamaa akihoji matokeo ya mkutano wa leo wa vyama tofauti vya kisiasa ndiyo yatakayoamua nani ana haki ya kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa ulaya.

Barroso asihi nafasi zaidi za kazi zibuniwe na kuhimiza ukuaji wa kiuchumi

Viongozi wa serikali na taifa wa mataifa 28 wanachama wa Umoja wa ulaya watakutana mjini Brussels kutathmini kishindo kilichotokana na uchaguzi wa bunge la ulaya pamoja pia na kuanzisha majadiliano kuhusu muundo wa halmashauri kuu ya Umoja huo.

Berlin Conference 2014 Jose Manuel Barroso
Mwenyekiti anaemaliza wadhifa wake Jose Manuel BarrosoPicha: picture alliance/AA

Akionekana kujibu kilio cha wapiga kura,mwenyekiti anaemaliza wadhifa wake Jose Manuel Barroso ametoa wito wa mshikamano na kubuniwa mkakati jumla ili kutetea "maadili na masilahi ya Ulaya" akiongeza mkakati muhimu zaidi ni kuhimiza ukuaji wa iuchumi na kubuni nafasi za kazi."

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir:AP/Reuters/AFP

Mhariri:Yusuf Saumu