Zidane: Bale anakaribia kuondoka Madrid | Michezo | DW | 22.07.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Zidane: Bale anakaribia kuondoka Madrid

Real Madrid wako nchini Marekani chini ya ukufunzi wa Zinedine Zidane. Na uvumi ambao umekuwa ukienea kwa muda mrefu kumhusu Gareth Bale hatimaye umefikia ukingoni.

Mkataba wa winga huyo na Real Madrid huenda ukamalizika katika siku chache zijazo. Zidane amesema klabu hiyo inafana juu chini kukamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu nyingine.

Bale, mwenye umri wa miaka 30, ameshinda mataji manne ya Ulaya tangu ajiunge na Madrid kutoka Tottenham Hotspur mwaka wa 2013 kwa rekodi ya kitita cha euro milioni 100, lakini akapata tabu sana kushirikishwa katika kikosi cha kwanza msimu uliopita.

Bale hakucheza katika mechi ya kirafiki dhidi ya Bayern Munich Jumamosi wakati Madrid walifungwa 3 -1. Kuwasili kwa Eden Hazard kumefanya mambo kuwa magumu hata zaidi kwa Bale. Zidane aliiwaambia wanahabari baada ya mechi hiyo kuwa Bale hakucheza kwa sababu anatafutiwa klabu nyingine akaondoke. Na hilo litafanyika haraka iwezekenavyo