1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya Waziri wa Misaada ya Maendeleo G. Müller Afrika

Oumilkheir Hamidou
22 Agosti 2018

Waziri wa misaada ya maendeleo wa serikali kuu ya Ujerumani Gerd Müller ataanza ziara rasmi katika mataifa sabaa ya Afrika akipigania umuhimu wa biashara huru. Hata hivyo wataalam wanashuku kama ziara hiyo itasaidia

https://p.dw.com/p/33ZAv
Ruanda Bundesentwicklungsminister Gerd Müller in Kigali
Picha: picture-alliance/dpa/U. Grabowsky

Akihojiwa na DW, mtaalam mashuhuri wa masuala ya maendeleo ya kiuchumi toka chuo kikuu cha Leipzig, Professor Robert Kappel anahisi suala la kuanzishwa eneo la biashara huru  halistahiki tena kukamata mstari wa mbele kwasababu tayari biadhaa za Afrika zinaingia katika masoko ya Ulaya. Professor Robert Kappel anaendelea kusema :"Suala hapo ni kuhakikisha bidhaa za Afrika zinaruhusiwa kuingia katika masoko ya ulaya, yaani bila ya ushuru, bila ya kuwekewa viwango na kadhalika. Biashara kama hiyo tayari ipo. Inadhihirika kana kwamba waziri hakauarifiwa vyema. Kanda ya biashara huru ipo na bidhaa za Afrika zinaingizwa. Ndio maana vyombo vya habari vinamkosoa waziri kwamba hakuarifiwa vizuri.

Professor Kappel anahisi uhusiano wa kibiashara kati ya Ulaya na Afrika unakuwa ingawa si kwa manufaa ya Afrika. Katika wakati ambapo bidhaa kutoka Ulaya na hasa kutoka Ujerumani zinamiminika kwa wingi katika nchi nyingi za Afrika , bidhaa za Afrika zinazoingia Ulaya zinapungua. Hali hiyo inatokana zaidi na bei anasema mtaalam huyo wa masuala ya maendeleo ya kiuchumi kutoka chuo kikuu cha Leipig, Robert Kappel anayataja mafuta na gesi ya ardhini kuwa sehemu kubwa ya bidhaa za Afrika zinazoingia katika soko la Ujerumani na Ulaya kwa jumla na kufuatwa na bidhaa za kilimo. Bei za  mazao ya kilimo na mafuta na gesi zimepungua miaka ya hivi karibuni.

Waziri wa misaada ya maendeleo Gerd Müller akitembelea kampuni ya Ibero Uganda,alipokuwa ziarani mwaka 2017
Waziri wa misaada ya maendeleo Gerd Müller akitembelea kampuni ya Ibero Uganda,alipokuwa ziarani mwaka 2017Picha: Imago/Photothek

Kizingiti cha ruzuku kwa bidhaa za kilimo za Ulaya

Kwa mujibu wa shirika la kuhimiza biashara na uwekezaji nchini Ujerumani, biashara ya nje ya Ujerumanai pamoja na nchi za Afrika kusini mwa jangwa la Sahara imeongezeka na kufikia Euro bilioni 26.1 mwaka jana. Na ile ya nchi hizo kuelekea Ujerumani imepungua kwa asili mia moja nukta moja kama ilivyokuwa mwaka mmoja kabla.

Kizingiti kikubwa kinatokana na ruzuku zinazotolewa na Umoja wa ulaya kwa bidhaa za kilimo. Professor Kappel anasema katika mahojiano yake na DW waziri wa misaada ya maendeleo anafanya kana kwamba kizingiti hicho hakipo. Ameshauri mataifa ya Afrika yawalipe ruzuku wakulima wao pia, lakini anasahau ruzuku hizo haziwezo kushindana na zile za Umoja wa Ulaya anasisitiza mtaalam huyo.

 

Mwandishi:Cascais Antonio/Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Josephat Charo