1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya Steinmeier Irak ina shabaha gani ?

18 Februari 2009

Msukosuko wa Opel na ziara ya Irak ndio mada kuu leo.

https://p.dw.com/p/GwdJ
Rais wa Irak na Bw.SteinmeierPicha: AP

Safu za maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo, zimegusia mada mbali mbali tangu za ndani hata za nje ya nchi: Nje, zimechambua ziara ya kwanza ya waziri wa nje wa Ujerumani Bw.Steinmeier nchini Irak na ndani msukosuko uliovikumba viwanda vya magari vya Ujerumani kama Opel na jinsi ya kuviokoa kufilisika.

Ramadhan Ali amewakagulia safu za wahariri hao na anaanza na gazeti la

Wetzlarer Neue Zeitung likiandika:

"Siasa mpya ya nje ya Marekani inalingana mno na ile ya chama cha Social Democratic Party ambayo ikiegemea upinzani wa vita vya Irak wa Kanzela wa zamani Gerhard Schroder na kuendelezwa hadi leo na Bw.Steinmeier aliekua waziri katika afisi ya kanzela wakati ule.

Hakuna mwengine anaeweza basi, kuwakilisha bora zaidi mwanzo mpya wa siasa ya Ujerumani kuelekea Irak kama Bw.Steinmeier."

Ama gazeti la Badische Zeitung likitubakisha katika mada hii laandika:

"Kuanzia sasa Ujerumani inaazimia kuiungamkono Marekani kwa nguvu zaidi kuliko ilivyokua hadi sasa.Kwani, tofauti na mtangulizi wake George Bush, rais Obama ametangaza kushauriana na washirika wake muhimu wa magharibi juu ya maswali muhimu ya kimataifa.Hata kuelekea ulimwengu wa kiarabu ,Obama anafuata mkondo mpya na ameahidi kuheshimiana....."Chini ya msingi huu, Bw.Steinmmeier amefungua njia ya siasa mpya kwa Irak na hivyo , amemnyoshea mkono wa kumsaidia Obama katika kuijenga upya Irak."

Kwa maoni ya gazeti la Oldenburgrische Volkszeitung - waziri wa nje wa Ujerumani Bw. Steinmeier katika kuzuru Irak, ametupia macho masilahi ya kiuchumi.Gazeti laandika:

"Irak iliovurugwa kwa vita,inatoa fursa kwa viwanda vya Ujerumani kuvuna fedha nyingi wakati huu wa msukosuko mkubwa wa kiuchumi ulimwenguni.Ikiwa hii itazisaidia pande zote mbili, hiyo basi ni biashara isio na dhambi hata ikionekana ni kiroja cha mambo kuwa, serikali ya zamani ya Ujerumani ya chama cha kijamaa cha SPD na kile cha mazingira cha Kijani miaka 6 iliopitaa haikukosea kupinga vita vya Marekani nchini Irak,lakini sasa inataka kufaidika na matunda ya vita vile."

Likitugeuzia mada,gazeti la Main-Post linauchambua msukosuko wa kiwanda cha magari cha Opel likiandika:

"Katika kutatua msukosuko wowote ,daima huwapo hatua mojawapo muhimu ya kuchukua:Kwa Ujerumani, hatua hiyo ni juu ya kiwanda cha Opel na Schaefler.Msaada unaoingia akilini na labda kushiriki kiasi fulani kwa serikali katika mradi wao,kungeweza kuviokoa viishi.

Kwani, kufilisika kwa viwanda vya ukubwa wa aina hii,kutageuka msukosuko mkubwa kuwa balaa lisilodhibitika tena.Hapa si swali la mustakbali wa viwanda vya motokaa vya Ujerumani,bali ni swali la hatima ya Ujerumani kama dola kuu la kiuchumi.Serikali ya Ujerumani kamwe isiviwache viwanda vya Opel na Schaffler kuzama."