Ziara ya rais Horst Köhler wa Ujerumani nchini Nigeria. | Matukio ya Kisiasa | DW | 11.11.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Ziara ya rais Horst Köhler wa Ujerumani nchini Nigeria.

Rais wa Ujerumani Horst Köhler aendelea na ziara nchini Nigeria.

default

Rais Horst Köhler wa Ujerumani na rais Umaru Yar Adua wa Nigeria.


Rais wa Ujerumani Horst Köhler anaendelea na ziara nchini Nigeria ametembelea mji wa Lagos na jimbo la Kano.

Rais Köhler ambae tayari amefanya mazungumzo na rais Yar Adua wa Nigeria amesema ni muhimu kwa Nigeria kupeleka maendeleo katika sehemu za mashambani vilevile.

Ameeleza kuwa ili kufikia shabaha hiyo pana haja ya kuendeleza miundombinu itakayowawezesha wakulima wadogo wadogo kufikisha mazao yao sokoni. Amesema ni kwa njia hiyo tu kwamba itawezekana kupambana na umasikini kwa ufanisi nchini Nigeria.

Kiongozi huyo wa Ujerumani anaefanya ziara ya nne barani Afrika pia ameitaka jumuiya ya kimataifa isaidie katika harakati za kupambana na rushwa inayosababisha utajiri wa Nigeria kushindwa kuwanufaisha watu wake wengi.

Rais huyo ameshauri kuwekwa kwa utaratibu utakaozuia wizi wa mafuta ya Nigeria.
 • Tarehe 11.11.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FrVo
 • Tarehe 11.11.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FrVo
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com