Ziara ya Pope Jordan na Israel | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 08.05.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Ziara ya Pope Jordan na Israel

Pope ziarani katika maeneo matakatifu

default

Baba Mtakatifu Benedikt wa 16, mkuu wa kanisa katoliki duniani


Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Benedict wa 16, leo hii anaanza ziara ya siku nane huko maeneo ya Mashairiki ya Kati.


Ziara hiyo ya kwanza kufanyika katika maeneo hayo inatajwa kubeba ujumbe wa amani pamoja na kufanya hija.


Tathimni inanoesha kuwa ziara hiyo ya siku nane itakabiliwa na mambo magumu katika masuala ya kidini pamoja na changamoto za kisaisa.

Papa, mwenye umri wa miaka 82, kituo chake cha kwanza kitakuwa Amman, mjini Mkuu wa Jordan, na baadae Israel, kisha katika himaya ya Wapalestina.

Mwanzoni mwa wiki hii alinukuliwa akisema jambo kubwa katika ziara ni kufanya hija ya amani.

Jambo la kwanza linarotajajiwa kufanyika nchini Jordan ni kukutana na Mfalme Abdullah wa Pili na atawatembelea Walemavu katika mji mkuu wa nchi hiyo.

Pia anatagemewa kuliibua suala la Wairaq ambao ni Waumini wa Dini ya Kikatoliki waliyo wachache.

Katika ziara yake hiyo imeelezwa atazungumza na Wapalestina katika kambi moja ya wakimbizi huko Bethlehem, ambako inaaminika kuwa ndipo alipozaliwa Yesu.

Miongoni mwa mambo mengine ambayo pia yatajwa kuwa Kiongozi huyo ya Kanisa Katoliki kuwa atayafanya huko Bethlehem ni kutembelea watoto waliyo hospitali.

Wakati ziara hiyo Papa mwenyewe akiita kama ya kiimani zaidi, lakini wachambuzi wanasema inahusiana sana na masuala ya kisiasa na kidiplomasia.


Kiongozi mmoja wa huko wa Kikatoliki huko Jerusalem, Fuad Twal, alinukuliwa katika televisheni ya akisema kila jambo,kila ishara inaonesha ziara ya kiongozi huyo wa kanisa katoliki itahusisha siasa.


Papa huyo wa Kijerumani anal engo la kuwasilisha ujumbe wa matumani kwa Waakristo katika nchi za Mashariki ya kati ili kupunguza vurugu zitokanazo na tofauti za kidini.

Chama kimoja cha Kiislam nchini nchini Jordan kimesema hawatampokea kiongozi huyo mpaka aombe radhi kutokana na kauli yake kuhusu Kuunganisha Uislamu na vurugu aliyoitoa mwaka 2006.

Katika matamshi yake Papa alimnukuu Mfalme wa Zamani wa Kikristo ambae alikosoa mafundisho ya Mtume Muhammad kama ya kishetani na si ya kibinadamu.

Kauli hiyo ilizusha chuki na hasira kutoka Waumini wa Dini ya Kiislamu Duniani kote.

Hata hivyo, Papa huyo aliwahi kuomba radhi kwa kusema hayakuwa matamshi yake, isipokuwa ilikuwa nukuu.

Kiongozi wa Chama hicho, Zaki Bani Rashed, amesema wanataka mabadiliko katika sera zake ili kurejesha amani katika maeneo hayo.

Israel ya sasa kwa mtazamamo wa kitamaifa inaonekana kama eneo la ubaguzi na uhalifu ambao umekuwa ukiendelea tangu mwaka 1948.


Mwandishi; Sudi Mnette/AFPE

Mhariri: Miraji Othman

 • Tarehe 08.05.2009
 • Mwandishi Sudi Mnette
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/HlzK
 • Tarehe 08.05.2009
 • Mwandishi Sudi Mnette
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/HlzK
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com