Ziara ya kiongozi wa kanisa katoliki nchini Marekani | Magazetini | DW | 21.04.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Ziara ya kiongozi wa kanisa katoliki nchini Marekani

"Amekwenda kama Hajj,amerejea kama mwanamuziki nyota"-wanasema wahariri

Papa Benedikt wa 16 mbele ya Ground Zero-mjini New-York

Papa Benedikt wa 16 mbele ya Ground Zero-mjini New-York


Mijada kuhusu malipo ya uzeeni,ziara ya kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Benedikt wa 16 iliyomalizika jana nchini Marekani na jinsi serikali ya Zimbabwe inavyowakandamiza wapinzani ndizo mada zilizochambuliwav zaidi na magazeti ya Ujerumani hii leo.


Tuanze basi na kumalizika ziara ya kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Benedikt wa 16.Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINER linaandika:


Alijihisi kama yuko nyumbani kabisa,Papa Benedikt wa 16 wakati wa ziara yake nchini Marekani.Ameonyesha kujivunia heshma na upendo.Kilichosababisha ziara ya kwanza ya kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni nchini Marekani kutajwa kua ziara ya kihistoria ni ile namna Papa Benedikt wa 16 alivyoonesha kuhuzunishwa mno na kashfa ya kunajisiwa watoto.

Takriban katika hafla zote,Papa Benedikt wa 16 alizungumzia masikitiko yake na jinsi makasisi hao walawiti walivyosababisha machungu na madhara kwa maelfu ya wahanga wao na kanisa pia."Pope of Hope" "Papa wa matumaini"-ndilo jina Benedikt wa 16 alilopewa na vyombo vya habari vya Marekani.Ni jambo la kutegemea kwamba mwito wake wa matumaini utaitikwa na kulifaraji pia kanisa katoliki la Marekani linalokumbwa na mizozo na mashaka."


Hayo ni maoni ya FRANKFURTER ALLGEMEINER ZEITUNG."Amekuja kama "Hajj amerejea nyumbani kama mwanamuziki nyota" hicho nddicho kuichwa cha maneno cha gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linaloendelea kuandika:


"Ni nadra kwa Papa Benedikt wa 16 kushuhudia shangwe kama zile.Amekabiliana kwa moyo mkubwa na kishindo kinacholikumba kanisa lake mwenyewe nchini Marekani.Hakutaka pia kupaza sauti kulionya dola kuu la magharibi.Kila mtu anatambua bora kujikosoa kuliko kukosolewa.Papa Benedikt wa 16 amedhihirisha nchini Marekani jinsi anavyoliangalia jukumu lake.Anajiangalia kama Mchungaji mkuu wa kiroho na mlinzi.Hataki kua kiongozi wa kidini anaejiingiza katika masuala ya kisiasa.Kwa kanisa pengine ni bora hivyo,lakini katika dunia patakosekana kiongozi ambae baadhi ya wakati atakua akiwatahadharisha wakubwa wa dunia hii."


Eneo la kusini mwa Afrika nalo pia lilimulikwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.Gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU limechamabua hali ya mambo nchini Zimbabwe na kuandika:


Kuna wanaolinganisha yanayotokea hivi sasa nchini Zimbabwe na hali namna ilivyokua Rwanda,kabla ya mauwaji ya halaiki ya mwaka 1994.Mtu anaweza kusema:"wanatia chunvi".Ukweli hata hivyo ni kwamba visa vya kikatili vinatokea katika nchi hiyo inayozongwa na mizozo.Wakosoaji wa serikali ya Robert Mugabe wanauliwa na wapinzani wanavunjwa mifupa ya mwili katika vituo vya mateso.Wengi wetu hatuna la kufanya isipokua tuu kuyatumbulia macho madhila yanayofanywa na Mugabe.Jumuia ya kimataifa haiwezi kuingilia kati kwasababu Zimbabwe si umuhimu-kwa hivyo tusifikirie kwamba patatokea siku ambayo wanajeshi wa kulinda amani watatumwa nchini humo.
►◄

 • Tarehe 21.04.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DlZM
 • Tarehe 21.04.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DlZM