Ziara ya Bush Africa | NRS-Import | DW | 16.02.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

NRS-Import

Ziara ya Bush Africa

Rais Bush atazamiwa kuwasili muda wowote leo hii Tz

DAR-ES SALAAMRais George W Bush wa Marekani anatazamiwa kuwasili nchini Tanzania muda wowote kutoka sasa katika zira yake ya siku sita barani Afrika ambayo itamfikisha pia nchini Ghana,Benin,Liberia na Rwanda.Akiwa safarini kuelekea Tanzani hapo jana rais huyo wa Marekani alisema mojawapo ya agenda zake ni kuzungumzia  uwezekano wa kuhamisha kikosi cha wanajeshi wa Marekani  kwa ajili ya Afrika kutoka Ujerumani na kukipeleka barani humo.Kiongozi huyo wa Marekani anatazamiwa kutafuta uungaji mkono wa viongozi wa Afrika juu ya wapi kuundwe makao makuu ya kikosi hicho kipya cha Marekani kwa ajili ya Afrika kinachojulikana kama AFIRICOM ambacho kitafanya kazi kwa ushirikiano na wanajeshi wa Africa.

Hata hivyo masuala mengine muhimu ambayo yanampeleka Bush barani Afrika ni pamoja na kuitangaza sera ya Marekani ya nchi za nje ,usaidizi kwa watu walioathirika na maradhi ya Ukimwi na Virusi vya HIV,pamoja na masuala ya kibiashara.Migogoro ya jimbo la Darfur nchini Sudan na Kenya pia yamo kwenye agenda ya rais Bush.Rais Bush hatazamiwi kufika Kenya lakini amemtuma waziri wake wa mambo ya nje Condolezza Rice kusafiri Kenya kusaidia kutafuta mwafaka wa suluhu ya kisiasa  nchini humo.Hapo jana katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon alimtolea mwito rais Bush kuzungumza na viongozi wa Africa juu ya kuwasaidia raia kuondokana na Umaskini pamoja na ukosefu wa mahitaji muhimu na Elimu.Wakati huohuo mamia ya watanzania waliandamana katika barabara za jiji la Daresalaam hapo jana kupinga ziara ya rais huyo wa Marekani wakibeba mabango yaliyokuwa na maandishi makali ya kumpinga.Usalama umeimarishwa katika mji huo.

 • Tarehe 16.02.2008
 • Mwandishi Ramadhani Yusuf, Saumu
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/D8Nw
 • Tarehe 16.02.2008
 • Mwandishi Ramadhani Yusuf, Saumu
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/D8Nw
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com