1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky: Mataifa ya Magharibi hayaungana kuisaidia Ukraine

Amina Mjahid
25 Mei 2022

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema hii leo kwamba nchi za Magharibi zimeendelea kugawika kuhusu kiwango cha uungaji mkono kwa Ukraine kujilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi uliodumu kwa miezi mitatu

https://p.dw.com/p/4BruK
Schweiz | Jahrestagung des Weltwirtschaftsforums 2022 in Davos | Wolodymyr Selenskyj
Picha: Gian Ehrenzeller/KEYSTONE/picture alliance

Akizungumza katika mkutano wa jukwaa la kiuchumi duniani linalofanyika mjini Davos, Uswisi, rais huyo wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kwa sasa hauoni ushirikiano na Umoja wa nchi za Magharibi kuelekea ulinzi wa Ukraine dhidi ya mashambulizi ya Urusi, huku akisisitiza kuwa umoja unamaanisha silaha zaidi kwa Kyiv jambo ambalo hadi sasa hajalishuhudia.

Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya zimetoa silaha za mabilioni ya dola kwa Ukraine kusaidia kukabiliana na wanajeshi wa Urusi waliojihami kwa silaha nzito nzito. Lakini Ukraine inaendelea kutoa wito wa uungwaji mkono kikamilifu, kujiunga na muungano wa kijeshi wa Jumuiya ya kujihami NATO unaoongozwa na Marekani na kuwekwa marufuku ya ndege kuruka katika anga zake.

Ukraine: Zelensky ataka nchi yake ipewe silaha zaidi za kupambana na Urusi

Zelensky ameongeza  kwamba Ukraine inamshukuru Rais wa Marekani  Joe Biden kusimama pamoja na taifa hilo la zamani la kisovieti lakini akasema ungwaji mkono wa mataifa yalio karibu na Ukraine bado unajikokota.

Amesema Ukraine iko katika bara la Ulaya na wanahitaji nguvu iliyoungana ya bara hilo katika vita vyake na Urusi. Katika mkutano huo wa jukwaa la kiuchumi duniani Zelensky amegusia kutaka mazungumzo ya moja kwa moja na Rais wa Urusi Vladimir Putin na sio kupitia wapatanishi, huku akisistiza kuwa Ukraine itaendelea kupambana hadi itakaokoa maeneo yake yote yanayoshikiliwa na Urusi.

Kampuni ya Pfizer kutoa dawa zake kwa bei nafuu kwa mataifa masikini

Symbolfoto Anti-Covid-Pille Paxlovid von Pfizer
Nembo ya kampuni PfizerPicha: SvenSimon/picture alliance

Kando na hilo kampuni ya Pfizer imetangaza kutoa kiwango maradufu cha dawa ikiwemo chanjo ya COVID 19 kwa bei nafuu kwa mataifa masikini duniani.

Tangazo hilo lililotolewa katika mkutano huo wa Davos umenuiwa kupunguza mzigo kwa mataifa takriban 45 iliyo na viwango vya chini vya mshahara. Mataifa mengi yapo Afrika lakini Orodha hiyo inajumuisha pia Haiti, Syria, Cambodia na Korea Kaskazini.

soma zaidi: Kampuni ya Pfizer imesema dawa yake inapunguza makali ya virusi kwa asilimia 89

Msemaji wa kampuni hiyo Pam Eisele amesema dawa hizo ambazo tayari zinapatikana kwa urahisi Marekani na Barani Ulaya ni pamoja na dawa 23 na chanjo zinazotibu magonjwa ya kuambukiza, aina kadhaa za saratani na magonjwa mengine.

Mwezi huu shirika la afya ulimwenguni WHO lilitoa wito kwa kampuni ya Pfizer kuweka utaratibu wa matibabu yake ya COVID 19 kufikiwa kiurahisi katika mataifa masikini duniani.

Vyanzo: afp/reuters/ap