MigogoroUkraine
Zelensky aiomba NATO kuimarisha ulinzi kwenye maeneo yake
30 Novemba 2024Matangazo
Rais Volodymyr Zelensky amesema NATO inatakiwa kuutanua ulinzi wake hadi kwenye baadhi ya maeneo nchini humo ambayo bado yanadhibitiwa na Ukraine.
Zelensky amesema hayo siku ya Ijumaa katika mahojiano na kituo cha utangazaji cha Sky News cha nchini Uingereza.
Amesema wanatakiwa kufanya hivyo mara moja, na kuongeza, watatumia njia za kidiplomasia kuyarejesha maeneo yao yanayokaliwa na Urusi.
Amesema, mpango huo haukuzingatiwa hapo kabla kwa kuwa hakuna aliyewapendekezea rasmi.