1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelenskiy: Hakuna cha kudhoofisha vita dhidi ya Urusi

Sudi Mnette
2 Oktoba 2023

Siku moja baada ya bunge la Marekani kuridhia muswada wa fedha unaizuia pia fursa usaidizi wa Marekani kwa Ukraine, Rais Volodymyr Zelenskiy amesema hakuna kitakachoweza kudhoofisha mapambano ya nchi yake dhidi ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4X1qt
USA | Wolodymyr Selenskyj und Joe Biden
Picha: Presidential Office of Ukraine/picture alliance

Kandoni mwa yaliozungumzwa na Rais Zelensky,  waziri wake wa ulinzi Rustem Umerov alisema amepata uhakikisho kuhusu usaidizi zaidi wa kijeshi kuptia simu ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin.

Amesema pamoja na hakikisho hilo lakini pia aliandika katika ukurasa wake wa X awali uliofahamika kama Twitter kuwa mashujaa wa Ukraine wataendelea kupata uungwaji mkono katika uwanja wa mapambano.

Serikali ya Ukraine na juhudi za kurejesha msaada wa Marekani

Nae msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Ukraine alisema serikali ya Kyiv inafanya kazi na mshirika wake Marekani ili kuhakikisha uamuzi wa bajeti mpya unajumuisha fedha kwa ajili ya taifa lao  na kwamba msaada wa Marekanin utakuwa madhubuti.

Rais Zelenskiy, katika hotuba iliyorekodiwa mahusi kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya Watetezi hakulitaja moja kwa moja bunge la Marekani lakini alisisitiza dhamira yake ya kupigania ushindi. Na kuoneza kuwa hakuna mtu atakelizuia taifa lake.

Ulaya yataka bunge la Marekani kutafakari upya uamuzi wake

Ukraine Bradley-Panzerbesatzung an vorderster Front – Region Saporischschja
Askari wa Ukraine akiwa katika harakati za ukombozi wa kijiji cha RobotynePicha: Dmytro Smolienko/Ukrinform/abaca/picture alliance

Katika hatua nyingine Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, ametoa wito kwa bunge la Marekani kutafakari upya uamuzi wao kuondoa usaidizi wa fedha kwa Ukraine baada ya kuridhiwa muswada wa fedha wa muda mfupi unaolenga kunusuru kufungwa kwa shughuli za serikali ya shirikisho.

Akizungumza jana Jumapili mjini Kyiv baada ya mkutano wake na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Borrell amesema anadhani hatua hiyo, haitakuwa ya kudumu na katika siku zijazo Ukraine itaendelea kunufaika na msaada wa taifa hilo.

Sheria hiyo iliyoipitishwa Jumamosi inayolenga kuisaida serikali ya shirikisho ya Marekani kujiendesha hadi Novemba 17, imekiweka kando kifungu chenye kutoa nguvu ya msaada wa ziada kwa Ukraine, hatua ambayo ni kipuambele kwa Rais Joe Biden.

Somza zaidi:NATO yazidi kuiunga mkono Ukraine

Pamoja na hayo yote lakini maafisa wa Ukraine walionekana kutoa msisititzo wa kwamba uungaji mkono wa Marekani kwa Ukraine ungepaswa kuendelea licha ya sheria hiyo ya kunusuru shughuli za serikali ya Marekani.

Chanzo: RTR