Zelaya ajipenyeza kwa siri kurudi Honduras . | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 22.09.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Zelaya ajipenyeza kwa siri kurudi Honduras .

Manuel Zelaya arejea nchini kisirisiri,na serikali ya mpito yatangaza amri ya kutotoka nje.

default

Manuel Zelaya ,rais aliepinduliwa amerudi tena nchini Honduras lakini safari hii kwa kujipenyeza kwa siri.

TEGUCIGALPA.

Rais aliepinduliwa nchini Honduras Manuel Zelaya amerejea nchini humo kisirisiri na ameomba  hifadhi  kwenye  ubalozi  wa Brazil  katika mji mkuu  wa  nchi  hiyo Tegucigalpa.

Zelaya alierejea  nchini jana anapigania kurudi  katika mamlaka kwa njia ya maandamano  na mgomo wa nchini kote.

Bwana  Zelaya mwenyewe amehakikisha kwamba hapatakuwa na  matumizi  ya nguvu na  ametoa mwito wa  kufanyika  mdahalo baina ya  matabaka yote ya  jamii nchini Honduras.

Wakati huo huo kiongozi wa kipindi cha mpito nchini  Honduras ameutaka  ubalozi  wa Brazil umtoe bwana  Zeleya  na umkabidhi kwa serikali.

Na habari kutoka New York zinasema  waziri wa mambo ya nje wa Marekani  Hillary Clinton  ametoa mwito juu ya kufanyika mazungumzo  ili kuepusha  umwagikaji damu nchini Honduras wakati  serikali  ya mpito  imetangataza  amri  ya  kutotoka nje na  pia imefunga uwanja  wa ndege.

 • Tarehe 22.09.2009
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Jm1y
 • Tarehe 22.09.2009
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Jm1y

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com