Zarif afanya juhudi za kuokoa makubaliano ya kinyuklia | Matukio ya Kisiasa | DW | 14.05.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Zarif afanya juhudi za kuokoa makubaliano ya kinyuklia

Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Javad Zarif amesema nchi yake itahitaji uhakikisho kutoka mataifa mengine yenye nguvu  duniani iwapo iendelee kutekeleza mkataba wa kinyuklia wa mwaka  2015, baada ya Marekani  ikujitoa.

Waziri wa mambo  ya  kigeni  wa Urusi  Sergei Lavrov  alikutana  na  mwenzake huyo wa  Iran mjini Moscow  Jumatatu  kujadili kile  kinachoweza  kufanyika  kulinda makubaliano  hayo  na  Iran  baada  ya  uamuzi  wa  rais  wa Marekani Donald Trump kujitoa  katika  mkataba  huo. 

Pakistan Karachi - Iranischer Außenminister Mohammad Javad Zarif besucht Pakistan (Getty Images/AFP/A. Hassan)

Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif

Iran  jana  iliupa  Umoja  wa  Ulaya  siku  60 kutoa uhakikisho wa kuendelea  na  utekelezaji  wa  makubaliano  hayo  ya  kinyuklia baada  ya  uamuzi  huo  wa  Marekani kujitoa. "Lengo  lililokusudiwa la  mazungumzo  ni kupata  uhakikisho kwamba  maslahi  ya  watu  wa Iran, yatalindwa," Zarif  alisema  katika  mkutano  na  mwenzake  wa Urusi, Sergei  Lavrov, kwa  mujibu  wa  shirika  la  habari  la  Urusi TASS.

Lavrov alisisitiza  kwamba  Urusi  na  wadau  wengine  katika mkataba  huo  wa  kinyuklia  wanania  ya  kuuendeleza, ujumbe ambao  umerejewa  pia  katika  matamshi  kutoka  Umoja  wa  Ulaya yaliyotolewa  na  waziri  wa  masuala   ya  Ulaya  wa  Ujerumani Michael Roth.

"Shirikisho  la  Urusi  pamoja  na  washiriki  wengine  katika  mkataba huo  wa  kinyuklia, China, mataifa  ya  Ulaya, pia  wana maslahi halali  ambayo  yamo  katika  makubaliano  hayo  yaliyoidhinishwa  na baraza  la  Usalama  la  Umoja  wa  Mataifa, " alisema  Lavrov.

"Leo tunamatumaini  kuona ushiriki  wa  mataifa  ya  Ulaya, China, Urusi, Iran  na  Umoja  wa Ulaya  kwa  kutumia  utaratibu  uliopo kutoruhusu  kuporomoka  kwa  waraka  huu  muhimu, kutoruhusu kuivuruga  hali  katika  eneo  la  mashariki  ya  kati, kutoruhusu vitisho  vipya  katika udhibiti  wa  kusambaa  kwa  silaha  za kinyuklia."

Iran Teheran Besuch Boris Johnson (Getty Images/AFP/A. Kenare)

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Boris Johnson akimpokea waziri mwenzake wa Iran Javad Zarif (Kulia)

Russia  ambayo  ina  uhusiano  imara  na  Iran, ilikuwa  mpatanishi katika  kupatikana  kwa  makubaliano  hayo  ya  mwaka  2015 yenye lengo  la  kuizuwia  Iran  kujipatia  silaha  za  kinyuklia.

Katika  mkutano  mjini  Beijing  mwishoni  mwa  juma, waziri  wa mambo  ya  kigeni  wa  China Wang Yi alimuahidi Zarif kwamba China  itaendelea  kufanyakazi  kuendelea  na  makubaliano  hayo.

Waziri wa mambo  ya  kigeni  wa  Iran Mohammed Javad Zarif amesema  mpango  wa  pamoja  wa  kuchukua  hatua , uliotiwa  saini mwaka  2015 ulikuwa  katika  msingi  wa  uwiano  wa  majukumu  kati ya  upande  wa  Iran  na    kulinda  maslahi  ya  watu  wa  Iran  ikiwa  ni  pamoja  na  Marekani."

 Staatsminister für Europa - Michael Roth in Skopje (DW/K. Delimitov)

Waziri anayehusika na masuala ya Ulaya wa Ujerumani Michael Roth

Mpango wa pamoja  wa  kuchukua  hatua uko  katika  msingi  wa uwiano wa  majukumu  kati  ya  upande wa  Iran na  Ulaya  ikiwa  ni pamoja  na  Marekani. Baada  ya  Marekani  kujitoa  uwiano  huu uko  hatarini. Tunapaswa  kuona  vipi  tunaweza tunaweza kuulinda.

Mataifa  matatu ya  Ulaya, Ujerumani, Ufaransa  na  Uingereza yameomba  muda  wa  siku  90, duru mjini  Tehran zimesema. Suala hilo  linatarajiwa  kuzungumzwa  katika  mkutano  kati  ya  Zarif  na wenzake  wa  Umoja  wa  Ulaya  mjini  Brussels  kesho  Jumanne.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae

Mhariri: Iddi Ssessanga

 

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com