Zanzibar yaomboleza kifo cha Sheikh Bachu | Matukio ya Afrika | DW | 14.02.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Zanzibar yaomboleza kifo cha Sheikh Bachu

Mchana huu Zanzibar imemzika mmoja wa wanazuoni wake maarufu wa dini ya Kiislamu, Sheikh Nassor Abdullah Bachu, ambaye alifariki dunia jana (13.02.2013) baada ya kuugua zaidi ya mwaka mmoja.

Wanawake wakiomboleza Zanzibar.

Wanawake wakiomboleza Zanzibar.

Sheikh Bachu atakumbukwa kama ulamaa kijana aliyeleta mapinduzi makubwa kwenye mawazo ya dini ya Kiislamu visiwani Zanzibar na katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki, akihubiri tapo jipya la dini hiyo lililofahamika kama Ahlu Sunna, akiwa na lengo la kurudisha mfumo wa maisha ya Kiislamu kama ulivyoasisiwa na kiongozi wake, Mtume Muhammad (S.A.W), na pia kuupa Uislamu sura ya kimataifa.

Sudi Mnette amezungumza na Dokta Issa Ziddy ambaye alimfahamu vyema Sheikh Bachu katika uhai wake na anaeleza nini umma wa Kiislamu Zanzibar umekipoteza kwa kifo cha Sheikh huyo.

Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Josephat Charo

Sauti na Vidio Kuhusu Mada