1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zanzibar imezindua rasmi chanjo ya Covid-19

22 Julai 2021

Hatimae Serikali ya Zanzibar imezindua rasmi chanjo ya Covid-19 baada ya Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee Jinsia na Watoto Ahmed Nassor Mazrui kuanza kuchanjwa na kuwahimiza wananchi kuondoa khofu.

https://p.dw.com/p/3xsLd
Tansania Sansibar | Coronavirus | Impfung Ahmed Nassor Mazrui, Gesundheitsminister
Picha: Salma Said/DW

Chanjo hiyo aina ya Cinovac kutona nchini China ambayo tayari imo katika vituo maalum vya afya vilivyotengwa kwa kazi hiyo ikiwemo kituo cha Lumumba ambacho yeye alifika na kuanza kuhudumiwa. Jumla ya dozi 10,000 ya chanjo hiyo zimeshawasili.

Tangu mwezi uliopita kumeibuka mjadala juu ya chanjo ya virusi vya corona baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dokta Hussein Ali Mwinyi kukubali kupokea chanjo kwa ajili ya Watanzania msimamo ambao ni kinyume na mtangulizi wao Dokta John Pombe Magufuli ambaye aliikataa chanjo hizo ilipoanza kutumika duniani.

WHO-Zulassung für chinesischen Impfstoff Sinovac Biotech
Picha: Chaiwat Subprasom/SOPA Images /ZumaWire/dpa/picture alliance

Licha ya mjadala huo wananchi hasa wafanyabishara na watu mashuhuri wameanza kuchanja kimya kimya jamii zao hadi leo ambapo Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ametangaza rasmi kuanza kwa chanjo kwa Mtanzania yeyote aliyekuwa tayari kuchanja. Sheptuu Hafidh Khalfan na Zuhura Mgeni ni wafanyakazi wa taasisi za serikali wanawahamasisha wenzao wajitokeze kwenda kupatiwa chanjo hiyo.

Pamoja na chanjo ya Cinovac kutumika nchini wananchi wanapata changamoto kutokana na chanjo nyengine kutokukubalika katika nchi za Ulaya na Marekani.