1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZANUpf KUKUTANA

24 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFl

HARARE:

Viongozi mashuhuri wa chama-tawala nchini Zimbabwe ZANUpf wanatazamiwa kukutana siku chache zijazo kujadili mpango wa kuitisha uchaguzi mkuu mwakani na kuachana na shauri lililozusha mabishano la kuahirisha uchaguzi huo hadi 2010.Hii imeripotiwa na gazeti rasmi THE HERALD.

Rais Robert Mugabe aliouambia mkutano wa wanawacke wa chama chake cha ZANUpf jana kwamba kuna maridhiano makubwa chamani kwamba uchaguzi tangu ule wa Bunge hata wa rais ufanyike mwakani na sio 2010.

Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 83 hapo kabla alipendekeza kuahirisha uchaguzi wa rais hadi 2010.