1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu 10 wauawa shuleni Urusi

11 Mei 2021

Watu wasiopungua 11 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya mtu mwenye silaha kufyatua risasi kwenye shule katika mji wa Urusi wa Kazan mapema leo hii.

https://p.dw.com/p/3tF3d
Russland Kasan Schießerei im Gymnasium Nr. 175
Picha: Yegor Aleyev/Tass/dpa/picture alliance

Kwa mujibu wa video iliyosambazwa na shirika la habari la RIA imeonyesha watoto wawili wakiruka kutoka ghorofa ya tatu katika jengo la shule hiyo la gorofa nne huku milio ya risasi ikisikika. Soma Urusi kumuhamishia Navalny hospitali baada ya kushinikizwa

Baadhi ya mashirika ya habari ya Urusi yameripoti kuwa vijana wawili wenye bunduki wamehusika na mashirika mengine yakiripoti kuwa mfyatuaji risasi alikua pekee. 

Hata hivyo shirika la habari la RIA limesema kijana mmoja mwenye silaha mwenye umri wa miaka 19 alikuwa amekamatwa  huku picha zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha kijana mmoja akiwa amebanwa chini na polisi nje ya jengo la shule hiyo.

Bunduki iliyotumika imesajiliwa

Russland Kasan Schießerei im Gymnasium Nr. 175
Magari ya polisi, yakubewa wagonjwa na wazima moto nje ya shule ya KazanPicha: Roman Kruchinin/AP/picture alliance

Akithibitisha tukio hilo Gavana wa mkoa wa Tatarstan Rustam Minnikhanov amesema kijana aliyehusika amekamtwa na silaha aliyoitumia ilikuwa imesajiliwa kwa jina lake na wengine waliohusika wametambulika na uchunguzi unaendelea.

Haijabainika ikiwa wafyatuaji risasi wengine walitoroka, na pia lengo la shambulio hilo halijafahamika.

Shirika la Habari la Serikali TASS limenukuu mamlaka ya utekelezaji wa sheria ambayo imesema mshambuliaji wa pili katika shule hiyo huko Kazan ambaye alibaki ndani ya jengo la shule hio aliuawa. Soma Putin awaonya wanaoingilia masuala ya ndani ya Urusi

Inaarifiwa kuwa wanafunzi watano na mwalimu mmoja hadi sasa wamethibitika kupoteza maisha. Mamlaka za mji wa Kazan zimewaondosha wanafunzi wote waliobakia kwenye eneo hilo.

Madaktari, waziri wa afya, pamoja na magari 11 ya kubebea wagonjwa yametumwa kwenye shule hiyo.

Ufyatuliaji risasi shuleni ni nadra Urusi

Ufyatuliaji risasi shuleni ni nadra nchini Urusi. Tukio moja kuu ya lilifanyika mwaka 2018 katika eneo la Crimea lililotwaliwa kwa nguvu na Urusi kutoka Ukraine, wakati mwanafunzi katika chuo kikuu alipouwa watu 19 na baadaye kujipiga risasi mwenyewe.
K

awaida, matukio ya ufyatuaji risasi kwenye maeneo ya umma ni machache nchini Urusi kutokana na sheria kali za kudhibiti unuzuzi na matumizi ya silaha.

 

Vyanzo:Afp/Ap/Reuters