1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YEREVAN: Uchaguzi wa ubunge nchini Armenia

13 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2Z

Uchaguzi wa wabunge katika Jamhuri ya Armenia umesemekana ulikumbwa na udanganyifu.

Watu takriban milioni mbili na laki tatu ndio waliokuwa na haki ya kupiga kura nchini humo lakini kiasi asili mia hamsini na tano ya idadi hiyo ndio waliojitokeza kwa uchaguzi huo.

Tume ya uchaguzi imesema inachunguza madai kadhaa yaliyowasilishwa rasmi.

Huo ndio uchaguzi wa nne wa taifa hilo lililopata uhuru wake mwaka 1991.

Wachunguzi wa kimataifa walisema uchaguzi uliopita wa mwaka 2003 ulikuwa umekiuka kanuni za kidemokrasia.

Kabla ya uchaguzi wa mwaka huu, mataifa ya magharibi yalitishia kukabiliana vikali na Armenia iwapo haitazingatia kurekebisha hali.