1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yemen:Hofu yatanda kutokana na mashambulizi ya anga

Zainab Aziz
4 Desemba 2017

Ni wazi kwamba ushirikiano hamna tena kati ya kundi la waasi wa Houthi na vikosi vinavyomtii Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdallah Saleh na hali hiyo inaashiria mabadiliko katika mgogoro wa Yemen.

https://p.dw.com/p/2oiL2
Jemen Sanaa Kämpfe
Picha: Reuters/M. al-Sayaghi

Usiku wa kuamkia leo wakaazi katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa walijawa na hofu kutokana na mashambulizi ya anga yaliyoendelea usiku kucha katika mapigano kati ya waasi na wafuasi wa rais wa zamani Ali Abdullah Saleh.

Hata hivyo msemaji wa muungano wa majeshi yanayoongozwa na Saudi Arabia jenerali Ahmed Assiri hajatoa tamko rasmi kuhusiana na mashambulio hayo. Chanzo kimoja kutoka uwanja wa ndege wa Sanaa kimefahamisha kuwa mashambulizi hayo yalilenga hususan maeneo ya waasi na kwamba uwanja huo wa ndege uko salama.Hadi sasa watu watu wapatao 60 wamuwawa katika mapigano hayo. Yemen imegawanyika kwa kati ya majeshi na serikali ya rais Abedrabbo Mansour Hadi katika eneo la kusini. Mansour Hadi anaungwa mkono na Saudi Arabia na anatambuliwa na Jumuiya ya Kimataifa, na kwa upande wa kaskazini kuna waasi wa Houthi na vikosi vinavyomuunga mkono rais wa zamani Ali Abdallah Saleh mwenye ushawishi mkubwa.

Rais wa Yemen Abedrabbo Mansour Hadi
Mbele: Rais wa Yemen Abedrabbo Mansour HadiPicha: Getty Images/AFP/E. Hamid

Kutokea mwaka 2014 mji mkuu Sanaa umekuwa unatawaliwa kwa makubaliano baina ya rais huyo wa zamani Saleh na waasi wa Houthi walioifurusha serikali ya Mansour Hadi na kisha kuanzisha serikali yao na kwa kipindi cha miaka miwili kwa pamoja na vikosi vya Ali Abdallah Saleh wamekuwa wanapambana na muungano wa majeshi yanayoongozwa na Saudi Arabia.

Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdullah Saleh
Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdullah SalehPicha: picture-alliance/AP Photo/H. Mohammed

Lakini baada ya rais huyo wa zamani kutangaza kwamba sasa yuko tayari kufungua ukurasa mpya akiwa na maana kuwa anataka kufanya mazungumzo na utawala wa Saudi Arabia. Hatua hiyo ya Saleh ndiyo imesababisha mgawanyiko huo na kuongeza chuki kati yake na waasi wa Houthi.  Mgogoro huo umesababisha hofu ya kuzuka mapinago mapya katika nchi hiyo inayokabiliwa na machafuko. Watu wapatao 8,750 wameuwawa tangu majeshi yanayoongozwa na Saudi Arabia yalipoanza operesheni yake nchini Yemen.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio GuterresPicha: Reuters/L. Jackson

Mgogoro huo umezidi kuitumbukiza Yemen katika hali mbaya ya ukosefu wea chakula na mahitaji ya msingi kwa binadamu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezihimiza pande zote kuacha mapigano ili kutoa njia ya kuifikisha misaada.

 

 

 

Mwandishi:Zainab Aziz/AFPE/APE

Mhariri:Yusuf Saumu