Yemen na mapatano ya kuacha mapigano | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 12.02.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Yemen na mapatano ya kuacha mapigano

Waasi kutimiza masharti 5

Ramani ya Yemen

Ramani ya Yemen

JESHI LA YEMEN :

Jeshi la Yemen, limetangaza kwamba mapigano yamesimamishwa katika safu zote za vita kati ya majeshi ya serikali na waasi wa madhehebu ya shiia wa kabila la Huthi.Hatua hii imefikiwa miezi 6 tangu serikali ya Yemen, kuanzisha hujuma kali ili kuzima uasi wa miaka 6 wa waumini wa madhehebu hayo huko kaskazini.Serikali ikiwatuhumu waasi wa kishia, kutaka kurejesha utawala wa Imam Zaidi uliotawala Sanaa,mji mkuu wa Yemen, hadi mapinduzi ya 1962 yalioigeuza nchi hiyo Jamhuri na kusababisha vita vya kienyeji vya miaka 8.

Rais Ali Abdullah Saleh wa Yemen, alitangaza kusimamishwa mapigano usiku wa manane hapo jana na Kiongozi wa waasi Abdul Malak al-Huthi, akawataka wapiganaji wake kuheshimu tangazo hilo.Makamanda wa jeshi la serikali waliarifu kuwa, wamewaona waasi wakiondosha vizuwizi vya njia walivyokuwa wameviweka katika njia-panda zinazoelekea milimani upande wa kaskazini wa Yemen,hii ikiwa hatua ya kwanza ya kutimiza masharti ya mapatano ya kusimamisha mapigano.

MASHARTI YA KUACHA MAPIGANO:

Mapatano hayo ya mambo 6,yanawataka waasi kufungua njia kuu 3 katika awamu ya kwanza ya kutimiza mapatano .Njia kati ya Saada,Harf Sufian na mji mkuu Sanaa.Njia inayotoka Saada ya magharibi kwendea Malahidh na njia kutoka mashariki ya Saada hadi Al-Jawf.Makamanda hao wamearifu kuwa ,wamewaona pia wapiganaji wa waasi wakiondoa mabomu yaliofukiwa chini ya ardhi kandoni mwa baadhi ya maeneo yao.

WASI WASI:

Lakini, katika ishara moja ya kuwapo bado shaka shaka na wasi wasi, afisa wa jeshi la serikali ameliambia shirika la habari la AFP kwamba , anasubiri kuona iwapo kweli waasi wataheshimu mapatano .Ni jana tu , pale afisa wa serikali ya Yemen, alipoliarifu shirika hilo la AFP kwamba, wanajeshi 12 wa serikali na waasi 24 wameuwawa katika mapambano makali katika jimbo la Amran,kaskazini mwa mji mkuu Sanaa.Duru ya mwisho ya mapigano ilizuka pale waasi walipohujumu ghafula wilaya ya Bukrat al-Shamsi juzi Jumatano.

Serikali ya Yemen awali, ilitoa masharti 5 ili kuafikiana kusimamisha mapigano: waasi wayahame majengo ya serikali,warejeshe silaha walizozinyakua kutoka majeshi ya serikali,wawaache huru wafungwa wao wote pamoja na wasaudi na wavihame vituo vya jeshi la serikali walivyo viteka na kufungua njia walizozifunga .Maafikiano juu ya mpango huu wa kuacha mapigano, yaliakhirika kwavile, serikali iliongeza sharti moja zaidi :kuwa waasi waache kuishambulia Saudi Arabia.

WASAUDI:

Wasaudi walijiounga na vita hivi Novemba mwaka uliopita baada ya kuwatuhumu waasi kumua mlinzi wao wa mpaka na kuviteka vijiji 2 vya Saudia.Vikosi vya nchikavu na ndege zake za kivita, vikpambana mara kwa mara na waasi.Serikali ya Yemen, ikiwatuhumu waasi hawa wa madhehebu ya shiia kutaka kurejesha utawala wa kiimam ,wa Imam Zaidi uliotawala mji mkuu wa Sanaa hadi ulipopinduliwa na mapinduzi ya 1962 yalioigeuza Yemen, Jamhuri na Waasi ambao tangu 2004 wamekuwa wakilalamika kubaguliwa wafuasi wa Zaidi wa kishiia tangu kiuchumi , hata kisiasa wakikanusha tuhuma hizo pamoja na kuwa eti wanapewa misaada ya kijeshi na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mwandishi: Ramadhan Ali/AFPE

Mhariri: Abdul-Rahman

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com