1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YANGON:Wanaharakati 4 maarufu wakamatwa

14 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7G2

Uongozi wa kijeshi nchini Myanmar umewakamata wanaharakati 4 wa kisiasa walio maarufu hata baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kushtumu vitendo vya kuwashambulia waandamanaji wanaodai demokrasia.Mmoja wa wanaharakati waliokamatwa ni Htay Kywe aliyeongoza baadhi ya maandamano ya mwanzo majuma kadhaa yaliyopita kabla kutoroka n akujificha ili kuepuka msako wa waandalizi wa maandamano hayo kulingana na shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch.Wengine watatu waliosalia wanaaminika kuwa wanachama waliosalia wa kundi la 88 Generation lililoanzisha mapinduzi ya demokrasia mwaka ’88.

Wanaharakati hao wanaaminika kusakwa na kukamatwa mjini Yangon.Kisa hicho kinatokea siku moja kabla mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa Ibrahim Gambari kurejea barani Asia ili kujaribu kuhusisha serikali za mataifa jirani kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo la Myanmar.Mwandiplomasia huyo anapanga pia kurejea mjini Yangon.