1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yanga kileleni mwa ligi Tanzania

5 Desemba 2022

Bao Pekee la Feisal Salum Abdallah dakika ya 90 limeirejesha Yanga kileleni mwa ligi kuu soka tanzania Bara kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.

https://p.dw.com/p/4KV09
Mhindi Joseph
Picha: Noah Patrick/DW

Kocha Msaidizi wa Tanzania Prisons,Shaban Mtupa baada ya kupoteza mchezo huo anasema wanajipanga na mchezo ujao.
Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 35 katika mchezo wa 14 na kurejea kileleni mwa Ligi ikiizidi pointi moja Simba SC ambayo pia imecheza mechi moja zaidi, wakati Prisons inabaki na pointi zake 15 za mechi 15 nafasi ya 11.

Tayari Kikosi cha Yanga kimefunga safari ya  kuwafuta  Namungo katika mchezo wa ligi kuu mchezo ambao utachezwa Disemba 7/2022.

Nayo Timu  ya Simba SC imekamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga siku ya Jumamosi na kufikisha pointi 34.

Coastal Union baada ya kichapo hicho wanabaki na pointi zao 12 za mechi 14 nafasi ya 13 na huyu ni  Kocha wa Coastal Union, Yusuph Chipo akisema wamezidiwa uzoefu.

Wakati huo huo Azam Fc  wanachuana na Simba kuwania nafasi ya pili na Leo wameshuka dimbani saa kumi jioni kuvaana na maafande polisi tanzania katika mchezo wa kuhitimisha Raundi ya kwanza.

Raundi ya kwanza ya Ligi kuu soka Tanzania bara inatarajiwa kutamatika wiki na hii.

Ligi Kuu ya Wanawake 2022/2023 Raundi ya Kwanza inatarajiwa kuanza kutifua Disemba 6 2022 huku timu 10 zikishiriki ligi hiyo. Simba queens watafungua dimba Disemba 6 kwa kucheza na Jkt Queens.

 

//Mhindi Joseph- Dar-es-Salaam