1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Xi asema uhusiano wa China na Urusi ni wa thamani kubwa

Josephat Charo
15 Aprili 2026

Rais wa China Xi Jinping amesema kwamba utulivu na uhakika wa uhusiano wa China na Urusi ni wa thamani hasa katika mazingira ya kimataifa yanayoambatana na mabadiliko na machafuko.

https://p.dw.com/p/5CCNA
Xi: Uhusiano wa China na Urusi ni wa thamani katika muktadha wa sasa wa kimataifa
Xi: Uhusiano wa China na Urusi ni wa thamani katika muktadha wa sasa wa kimataifaPicha: China Daily/REUTERS

Akizungumza Jumatano wakati wa mkutano na waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergey Lavrov, huko Beijing,rais wa China, Xi Jinping amesema mwaka huu unaadhimisha miaka 30 ya ushirikiano wa kimkakati wa China na Urusi na kumbukumbu ya miaka 25 ya Mkataba wa Ujirani Mwema na ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Urusi.

Xi alisema chini ya mwongozo wa kimkakati wa yeye na rais Putin kwa miaka mingi, ushirikiano wa kimkakati wa kina wa China na Urusi umedumisha maendeleo ya kiwango cha juu na matokeo ya ushirikiano yenye matunda katika nyanja mbalimbali.

Pia alisema katika mazingira ya kimataifa yaliyojaa mabadiliko na machafuko, utulivu na uhakika wa uhusiano wa China na Urusi ni wa thamani sana, na uhai mkubwa na umuhimu wa mfano wa mkataba wa ujirani mwema na ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Urusi ni muhimu zaidi.

Rais Xi amesema China na Urusi zinahitaji kutumia ushirikiano wa kimkakati wa karibu na wenye nguvu ili kutetea maslahi halali ya mataifa yote mawili na kulinda umoja wa nchi za kusini mwa dunia. Pia ametoa wito kwa nchi hizo mbili kuonyesha uwajibikaji na kujitolea kwa mataifa makubwa na wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Lavrovanajiunga na Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez, Mwanamfalme wa Abu Dhabi, Sheikh Khaled bin Mohamed bin Zayed Al Nahyan, na kiongozi wa Vietnam, To Lam, katika mkutano na Xi wiki hii.