WTO yatoa ripoti yake | NRS-Import | DW | 22.07.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

NRS-Import

WTO yatoa ripoti yake

Ripoti hiyo ya Shirika la Biashara Duniani inaelezea mifumo halali ya biashara.

default

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), Pascal Lamy.

Shirika la Biashara Duniani (WTO), limesema kuwa usalama wa mifumo halali ya kibiashara inayoruhusu nchi kusimamisha au kutupilia mbali biashara, unaweza kuharibu uchumi wa dunia kama utatumiwa vibaya kwa masuala ya kujilinda kwa kuzifanya nchi kuhimiza wananchi wake kununua bidhaa za ndani.

Katika ripoti yake ya mwaka, WTO, imechunguza matumizi ya hatua za dharura, mada iliyokuwa hasa muda muafaka kuonyesha wasiwasi wa kujilinda wakati wa msukosuko wa kiuchumi. Shirika hilo linaloangalia biashara ya dunia nzima, limekuwa likifatilia hatua za vizuizi zinazochukuliwa na nchi mbalimbali hasa zile zinazokiuka makubaliano ya kibiashara na zile zinazoruhusiwa chini ya mikataba inayofanya kazi kwa sasa.

Katika tathmini ya hivi karibuni ya WTO iliyotolewa mwezi huu, Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Pascal Lamy, amesema serikali hazikuwa sawa kuzuia biashara, ikiwa ni katika kukabiliana na kushuka kwa biashara.

WTO imebaini kuwa ni rahisi kufatilia matukio yasiyotarajiwa kuliko kuonyesha hatua za kibiashara katika kuokoa uchumi na fedha za hazina ya serikali zinazotolewa na mataifa tajiri na zile zinazoinukia kiuchumi kama vile China na Brazil.

Lamy amesema kuwa kujilinda kunaweza kuzidisha mzozo wa kiuchumi, hata kama siyo sababu ya kushuka kwa biashara. WTO imechunguza hatua za vizuizi kama vile kujilinda, kutokubali kuingiza bidhaa nyingi na kulipwa sehemu ya ushuru iliyofidiwa na nchi zinazoingiza bidhaa.

Hatua nyingine ni pamoja na ahadi za kujadiliana kuhusu ushuru wa forodha, kusafirisha kodi na kuongeza ushuru kwa makubaliano yaliyofikiwa. Utafiti wa kiuchumi unaonyesha kuwa matumizi ya hatua hizo zinaongezeka zaidi wakati wa kushuka kwa biashara.

Kwa mujibu wa utafiti huo, kutoruhusu kuingizwa kwa wingi bidhaa kutoka nje inakuwa pale serikali inapoanzisha ushuru wa bidhaa zinazoingizwa, ikisema kuwa zitauzwa kwa bei ya chini kuliko bei iliyokuwa ikiuzwa nchi zilizotoka.Katika kesi ya hivi karibuni, China imepanga kushindana na Umoja wa Ulaya kutoingiza bidhaa nyingi nchini humo, hasa zile za vipuri na skrubu.

Hatua kama hizo zinazipa serikali fursa ya muda kutoka kibiashara na kuziruhusu serikali hizo kusaini kwa undani zaidi ufunguzi, huku zikipunguza ushindani wa kibiashara na kisiasa. Hatua hizo zinaziwezesha serikali hizo kubadilisha masharti ya kiuchumi, afya au mazingira au maendeleo ya teknolojia katika nchi za nje yanayoviweka viwanda vya ndani kuwa na kasoro.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya WTO, hata hivyo, hatua hizo zinalenga kukabiliana na matatizo ya kiwanda kimoja wakati zikipuuzia athari zake katika sekta ya uchumi, kwa ujumla.

Ripoti hiyo imetolea mfano hatua ya kuzuia uingizaji wa bidhaa nyingi, ambapo kunatoa muda kwa viwanda vya ndani, lakini zinawaumiza wateja na kampuni nyingine zinazotegemea kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi, ambapo huongeza bei ya bidhaa hizo.

Ripoti hiyo inaendelea kufafanua kuwa kulipwa sehemu ya ushuru iliyofidiwa na nchi zinazoingiza bidhaa, kunawasaidia wazalishaji wa ndani kuliko kunufaisha uchumi kwa ujumla.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo (IPS)

Mhariri: Othman Miraji

 • Tarehe 22.07.2009
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/IvRd
 • Tarehe 22.07.2009
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/IvRd

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com