Wolfsburg ndani, Moenchengladbach nje | Michezo | DW | 09.12.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Wolfsburg ndani, Moenchengladbach nje

Kulikuwa na kizaazaa cha michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya – Champions League, ambapo kulikuwa na kilio kwa walioshindwa na furaha kwa waliojikatia tikiti ya kutinga hatua ya 16 bora

Manchester United wakicheza ugenini dhidi ya VfL Wolfsburg ilisalimu amri baada ya kupata kichapo cha 3-2 na kuondolewa katika michuano hiyo,

Manchester City wakiwa nyumbani Etihad waliwavunja moyo Borussia Moenchengladbach wa Ujerumani kwa kupata ushindi wa 4-2 mabao ambayo yamefungwa na David Silva, Raheem Sterling na Bony Wilfried. Ushindihuo uliwaweka kileleni mwa kundi D.

Vinara wa kundi A Timu ya Real Madrid wakiwa nyumbani Santiago Bernabeu waliwazaba Malmo kutoka Sweden mabao 8-0 ambayo yalingwa na wachezaji karim Benzema mabao (3), Christiano Rolnado mabao (4) pamoja na Mateo kovacich bao (1).

PSG ya Ufaransa iliizidi nguvu Shakhtar Donetsk ya Ukraine kwa kuifunga 2-0, kupitia wachezaji Lucas Moura na Zlatan Ibrahimovic.

Michezo mingine PSV Eindhoven imeichapa 2 – 1 CSKA Moskova, Benfica ikalazwa 1 – 2 na Atletico Madrid, Galatasaray imetoka sare ya 1 – 1 na FC Astana, huku Sevilla ikishinda bao 1 – 0 dhidi ya Juventus.

Mechi hizo za makundi zitaendelea tena zinatarajia kuendelea tena hii leo kwa michezo mbalimbali ,na miongoni mwa mechi hizo niBayer Leverkusen na Barcelona, Olympiakos na Arsenal, Dinamo Zagreb na Bayern Munichi.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Mohammed Khelef

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com