1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wito kusaidia nchi masikini kupambana na ongezeko la joto

4 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CWg9

Wanaharakati katika mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa unaofanywa Bali nchini Indonesia,wametoa mwito wa kutumia mabilioni ya dola kuzisaidia nchi masikini kupambana na athari za ongezeko la joto duniani.

Wanaharakati hao wanayatuhumu madola tajiri kuwa hayasaidi vya kutosha na nchi masikini ndio huathirika zaidi kutokana na mafuriko,ukame na vimbunga kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Kiasi ya wajumbe 10,000 kutoka nchi 190 wanahudhuria mkutano huo wa siku 11,kwa majadiliano ya mkataba mpya wa hali ya hewa, utakaochukua nafasi ya ule wa Kyoto unaomalizika mwaka 2012.

Marekani ni nchi pekee tajiri iliyokataa kutia saini mkataba huo.Waandalizi wa mkutano huo wanataka Marekani ishiriki katika mkataba mpya.