William Burns atua Misri leo | Matukio ya Afrika | DW | 15.07.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

William Burns atua Misri leo

Duru za kiusalama na kitabibu nchini Misri zimeripoti watu watatu leo wameuawa na wengine 17 kujeruhiwa wakati watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo waliporipua basi lililomebeba wafanyakazi kaskazini mkoa wa Sinai Misri.

Naibu waziri wa mambo ya nje waMarekani William Burns

Naibu waziri wa mambo ya nje waMarekani William Burns

Walioshuhudia tukio hilo wamesema washambuliaji hao walisikika wakisema ''Allah Akbar'' kwa maana Mungu mkubwa! baada ya kushambulia basi hilo katika mji wa Al-arish eneo ambalo limeshuhudia mashambulizi makubwa ya wanamgambo wa kiislaamu tokea aliyekuwa Rais wa Misri Mohamed Morsi kupinduliwa madarakani na jeshi Julai 3 mwaka huu.

Akitowa taarifa kupitia mtandao wa kijamii Facebook msemaji wa jeshi la Misri amesema makundi ya kigaidi yalikuwa yamedhamiria kushambulia gari la polisi lakini hawakufanikiwa na hivyo kushambulia basi badala ya gari hilo la polisi.

Makundi ya wapiaganaji wenye itikadi kali za kiislaamu kaskazini mwa mji wa Sinai eneo ambalo hakuna sheria ambalo linapakana na Israel na ukanda wa Ghaza limeshuhudia mashambulizi dhidi ya polisi na askari kwa miaka miwili iliopita, hali ambayo imezorotesha usalama tokea vuguvugu lililomtoa madarakani Husni Mubarak.

Lakini machafuko katika mji huo yamezuka tena baada ya Morsi kuondolewa madarakani, na wanamgambo wa eneo hilo wanadaiwa kushambulia vituo vya usalama na maeneo mengine muhimu na kuuwa kwa uchache watu 13 na kujeruhi wengine kadhaa.

Msemaji wa chama cha udugu wa kiislaamu Ahmed Aref amekanusha madai hayo ya kuvuru amani katika mji wa Sinai na kudai kuwa machafuko hayo yanawezakuwa yanachochewa na jeshi la Misri.

''Matukio mabaya dhidi ya raia, polisi na jeshi katika mji wa Sianai ni mpango wa usalama wa taifa wa Misri ili kuvuruga maandamano ya amani ya watu wetu katika mji wa Sinai kupinga mapinduzi ya jeshi la Misri''amesema Kiongozi mkubwa wa chama hico Essam El-Elrian

Wafuasi wa Morsi wapinga zaiara ya Burns

Waandamanamaji

Waandamanamaji

b Huku hayo yakijiri,naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani William Burns leo anafanya mazungumzo na maafisa wa serikali inayoungwa mkono na Jeshi la nchi hiyo ili kurudisha serikali itakayachaguliwa baada ya kuondoka madarakani Mohamed Morsi, huku waandamanaji wakiapa kufanya maandamano makubwa,

William Burns anakuwa kiongozi wa kwanza wa Marekani kutembelea Misri tokea jeshi la nchi hiyo kumuondoa kiongozi wa chama cha udugu wa kiislaamu Mohamed Morsi. Katika mkutano huo Burns atasisitiza juu ya msaada wa marekani kwa watu wa misri, kumaliza machafuko yote na uatwala wa mpito kuelekea serikali ya kidemokrasia itakayochaguliwa na wananchi wa Misri.

Burns ambaye atakuwa mjini Cairo hadi kesho Jumanne, anakutana pia na wanaharakati wa kirai na wahanyabiashara.

Mwandishi: Hashim Gulana/AFP/DPAE& RTRE

Mhariri: Yusuf Saumu