Willi Orban wa RB Leipzig avunjika mkono | Michezo | DW | 05.03.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Willi Orban wa RB Leipzig avunjika mkono

Beki wa RB Leipzig Willi Orban amevunjika mkono na hatacheza mechi kadhaa, klabu hiyo ilisema Alhamisi. (04.03.2021)

Leipzig ilisema mchezaji huyo raia wa Hungary alijeruhiwa wakati wa mechi ya robo fainali ya kombe la shirikisho la Ujerumani DFB Pokal na Wolfsburg siku ya Jumatano. Orban tayari amefanyiwa upasuaji, ilisema klabu hiyo.

"Hataweza kucheza kwa siku kadhaa, lakini baadaye ataweza kucheza na kifaa cha kumlinda," ilisema Leipzig.

Orban atakosa mechi ya Bundesliga ugenini Freiburg Jumamosi (06.03.2021) lakini huenda akawa katika hali nzuri kuweza kucheza mechi ya duru ya pili ya kombe la mabingwa barani Ulaya wiki ijayo na Liverpool, katika hatua ya timu 16 bora.

(dpa)