Wikileaks | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 01.12.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Wikileaks

Interpol yatoa waranti ya kumkamata Julian Assange

default

Mmiliki mtandao wa Wikileaks Julian Assange.

Polisi ya kimataifa Interpol imemtaja Julian Assange mmiliki wa mtandao wa Wikileaks kuwa miongoni mwa watu wakuu inayowasaka. Waranti ya kukamtwa kwa Assange iliyotolewa na Interpol ina maana kwamba huenda Assange akakamatwa kokote. Hapo awali mmiliki huyo wa Wikileaks alikata rufaa dhidi ya amri ya kukamtwa kwake iliyotolewa na Sweden kwa kumtuhumu kwa ubakaji.

Mahakama ya mjini Stockholm ilitoa waranti ya kukamatwa Assange siku kumi zilizopita.Taarifa kuhusu aliko Assange hazijulikani.

Kwa upande wake Marekani inaonekana kufikiria kumshtaki mmiliki wa mtandao wa Wikileaks kwa makosa ya ujasusi baada ya mtandao huo kuchapisha nyaraka za siri za kidiplomasia kwa vyombo vya habari.

NO FLASH Wikileaks Logo

Ukurasa katika mtandao wa Wikileaks.

Huku hayo yakijiri, mtandao huo umesema umevamiwa na ulizimika kwa masaa katika nchi kadhaa hapo jana. Katika mahojiano  na jarida la Forbes, Assange amesema anapanga kulilenga soko la  hisa la Wallstreet Marekani mwaka ujao. Assange ambaye ni mzaliwa wa Australia, amesema amepanga kufanya ufichuzi mkubwa wa nyaraka zinazohusu taasisi moja kubwa ya kifedha Marekani, itakayofichua nyenendo haramu zitakazo sababisha kufungwa kwa benki moja au mbili.

Mwandishi: Maryam Abdalla/ Afp/Ap/Dpae

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com