Wikileaks yafichua uchambuzi wa Guantanamo | Matukio ya Kisiasa | DW | 27.04.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Wikileaks yafichua uchambuzi wa Guantanamo

Washukiwa ugaidi 20 wa kwanza kutoka jumla ya 776, walisafirishwa Guantanamo Januari 2002.Maafisawa kijeshi wa Marekani walichunguza uwezo wa kiakili wa wafungwa hao na uwezo wa kupanga au kufanya vitendo vya ugaidi.

epa02476446 (FILE) A file photograph showing Wikileaks founder Julian Assange speaking about his organization Wikileaks and the United States and the human rights, during a press conference, at the Geneva press club, in Geneva, Switzerland, 04 November 2010. Media reports state on 02 December 2010 that Sweden's top court has rejected an attempt by Wikileaks founder Julian Assange to appeal against a detention order issued for him over alleged sexual crimes. EPA/MARTIAL TREZZINI +++(c) dpa - Bildfunk+++

Mwasisi wa tovuti ya Wikileaks

Sasa tovuti ya Wikileaks imefichua habari zinazohusika na uchambuzi uliofanywa katika jela ya kijeshi ya Guantanamo. Baada ya ripota wa gazeti la New York Times, Scott Shane, kutumia majuma kadhaa kupitia ripoti za uchambuzi uliofanywa kuhusu maisha ya washukiwa hao, amesema kuwa mchakato huo wa uchambuzi ulikuwa mgumu sana. Ilikuwa kazi kubwa hata kupata kujua majina yao. Anasema, ukweli ni kwamba kulitokea makosa kwani hakuna alieweza kujitambulisha. Anasema:

"Ilikuwa shida pia kutofautisha kati ya mkulima masikini anaesema kuwa yeye ni mkulima tu na mfuasi wa Al-Qaeda anaejidai kuwa mkulima."

Kwa hivyo, wala haishangazi kuwa wachambuzi hao walifanya makosa. Lakini kilichowashtusha Wamarekani wengi ni jinsi maafisa wa kijeshi walivyoamini zaidi dhana kuliko ushahidi kamili. Na dhana hizo zilishawishi maamuzi ya serikali ya Bush kuhusu hatima ya wafungwa hao.

** FILE ** In this June 6, 2008 file photo, reviewed by the U.S. Military, the sun rises over Camp Delta detention compound at Guantanamo Bay U.S. Naval Base, in Cuba. The Supreme Court ruled Thursday, June 12, 2008, that foreign terrorism suspects held at Guantanamo Bay have rights under the Constitution to challenge their detention in U.S. civilian courts. (AP Photo/Brennan Linsley, Pool, File)

Jela ya Guantanamo ya jeshi la Marekani

Baadhi ya washukiwa hao waliachiliwa huru baada ya kuchunguzwa na kuaminiwa kutokuwa na hatia lakini muda mfupi baadae, walijiunga na harakati za itikadi kali. Wengine kama vile Murat Kurnaz, mkaazi wa Bremen Ujerumani, alihesabika miongoni mwa wale wenye hatari kubwa, lakini tangu kuachiliwa kwake, Kurnaz anaishi kwa amani.

David Reemes, wakili anaetetea wafungwa wa Guantanamo anathibitisha kile kilichofichuliwa na mtandao wa Wikileaks. Anasema, kuwa ni vigumu sana kubashiri wakati ambapo, ushahidi uliopo hauwezi kutegemewa, kwa hivyo wameamua kuambatana na hisia zao au yale yalioelezwa na wafungwa wengine.

Wizara ya ulinzi ya Marekani imethibitisha kuwa asilimia 14 ya wafungwa walioachiliwa huru kutoka Guantanamo sasa wamejiunga na harakati za ugaidi nchini Yemen, Afghanistan na Pakistan. Wengi wao, walidhaniwa kuwa si hatari hivyo kwa Marekani na washirika wake.

Hata wakili Thomas Willner alipoeleza kuhusu mfungwa mmoja wa Guantanamo aliemtetea, alisema kuwa baada ya mshukiwa huyo kuachiliwa huru, ameingia katika mazingira ya kigaidi nchini Afghanistan.Ameeleza hivi:

"Siamini kama alikuwa gaidi alipokamatwa na kufungwa. Lakini Guantanamo, imemfanya achanganyikiwe kiakili. Kwa muda wa miaka yote hiyo, kijana huyo aliekuwa mkimya, mwenye adabu akabadilika na kugeuka kuwa mkali na mwenye hasira. Nilishtuka sana."

Kwa upande mwingine, kisichojulikana, ni wangapi waliogeuka kuwa majasusi wanaoifanyia kazi idara ya upelelezi ya Marekani CIA.

Mwandishi: Hasselmann,Silke/ZPR/ P.Martin

Mhariri: Othman, Miraji

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com