Wieczorek-Zeul anaonya dhidi ya kupunguzwa misaada ya maendeleo | Habari za Ulimwengu | DW | 11.10.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Wieczorek-Zeul anaonya dhidi ya kupunguzwa misaada ya maendeleo

Waziri wa misaada ya maendeleo wa serikali kuu ya Ujerumani anashauri misaada ya maendeleo itolewe kama ilivyoahidiwa na mataifa tajiri kiviwanda


Washington:

Waziri wa misaada ya maendeleo wa serikali kuu ya Ujerumani bibi HeidemarieWieczorek-Zeul ameyaonya mataifa tajiri kiviwanda,mzozo wa fedha usije ukawa sababu ya kupunguzwa misaada kwa nchi maskini."Ni kwa masilahi ya nchi tajiri kiviwanda,ikiwa utaepukwa mwanya unaoigawa dunia sehemu mbili-masikini na matajiri-" amesema waziri huyo wa kutoka chama cha Social Democratic,mjini Washington."Hali kama hiyo itazidi kuchochea mizozo ambayo itazigharimu fedha nyingi zaidi nchi tajiri kuliko misaada yao ya maendeleo.Waziri Heidemarie Wieczorek-Zeul anategemea serikali kuu ya Ujerumani itatoa misaada ya maendeleo kama ilivyoahidi, licha ya mzozo wa fedha.Waziri Wieczorek Zeul alikua Washington kuhudhuria mkutano wa benki kuu ya dunia.

 • Tarehe 11.10.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FY4C
 • Tarehe 11.10.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FY4C
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com