1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yasema imeahirisha uamuzi wa kumchunguza Ghebreyesus

Saumu Mwasimba
24 Januari 2022

Afisa mmoja wa shirika la afya duniani WHO amearifu kwamba taasisi hiyo itaakhirisha kutowa uamuzi kuhusu ombi lililotolewa na Ethiopia, la kutaka imchunguze Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus

https://p.dw.com/p/460iA
WHO-Chef | Tedros Adhanom Ghebreyesus
Picha: Fabrice Coffrini/REUTERS

Ethiopia imemtuhumu Ghebreyesus kuhusika na hatua za kuunga mkono vikosi vya wapiganaji wa Tigray wanaopambana na serikali kuu ya Ethiopia.

Mwenyekiti wa bodi kuu ya utendaji ya WHO Patrick Amoth ametoa taarifa hiyo katika mkutano wa bodi hiyo mjini Geneva ambako hatua ya Ghebreyesus ya kutaka kuwania muhula wa pili WHO imepangwa kujadiliwa.

Amoth amesema ombi la serikali ya Ethiopia ni suala gumu lenye kubeba athari za kisiasa  na liko nje ya mfumo wa taratibu za kamati hiyo na kupendekeza suala hilo liwekwe kando,na kujadiliwa na wale wanaohusika katika wakati mwafaka.

Wanachama wote 34 wa WHO wa bodi hiyo wamekubaliana na mwelekeo uliotolewa. Katibu mkuu wa WHO mwanzoni mwa mwezi huu alisema msaada unazuiwa kuingia katika jimbo la Tigray ambako ndiko alikotokea na ambako vikosi vya wapiganaji wa TPLF wanapambana na wanajeshi wa serikali kuu.